• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AFAFANUA UKWELI WA KILICHOTOKEA SIKU YA MAZOEZI YA SIMBA-CCM KIRUMBA

Posted on: November 22nd, 2024

RC MTANDA AFAFANUA UKWELI WA KILICHOTOKEA SIKU YA MAZOEZI YA SIMBA-CCM KIRUMBA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amekanusha taarifa ya uongo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayotolewa na msemaji wa klabu ya Simba,Ahmed Ally kuwa ameingilia mazoezi ya Simba akiwa pamoja na askari wenye silaha na kuwataka wananchi na mashabiki kuipuuzia taarifa hiyo yenye nia ya kumchafua na kumvunjia heshima.

Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kuzungumza na vyombo vya habari mapema leo asubuhi Novemba 22,2024 Ofisini kwake baada ya kupokea ujumbe mwingi wa kuulizwa kuhusiana na uzushi huo,na kubainisha alichofanya yeye kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa ni kwenda uwanjani baada ya kupokea taarifa ya kutaka kupigwa na makomandoo wa Simba na kujifungia vyumbani  wasimamizi wa Pamba Jiji kwenye uwanja huo ili wasiumizwe na kuanza  kuvunja vioo vya madirisha.

Mtanda amesema anatambua kanuni za soka na asingeweza kuingia uwanjani wakati ilikuwa ni siku ya mazoezi ya Simba na badala yake alikuwa nje ya uwanja akifanya mawasiliano na baadhi ya viongozi wa Simba ili wazungumze kuachiwa wasimamizi wa Pamba Jiji waliokimbilia vyumbani kuhofia kupigwa na makomandoo wa Simba.


"Jitihada zangu za kuzungumza na viongozi wa Simba ziligonga mwamba nikiwa nje ya uwanja hadi walipomaliza mazoezi yao na mlango kufunguliwa na askari kuingia na kuwafikisha kituo cha polisi aliyevunja vioo vya madirisha na wasimamizi wa Pamba Jiji kwa maelezo zaidi",amefafanua Mkuu wa Mkoa.

Ameongeza kuwa kutokana na sakata hilo Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu baadaye alimpigia simu na kumuomba radhi kwa yote yaliyotokea na kuahidi kugharamia hasara iliyotokea ya uharibifu uwanjani hapo.


Mtanda amewaondoa hofu mashabiki wote na kuwataka kuendeleza mshikamano wa amani na kufurahia burudani ya kuzishuhudia timu kubwa za Simba na Yanga na kupuuzia uzushi huo ulioenezwa na msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally ambao una nia ya kuwapa taharuki mashabiki kuelekea mchezo huo utakayopigwa leo Novemba 22,2024 kwenue uwanja wa CCM Kirumba.

Aidha Mtanda amebainisha yeye ataendelea kuwa mlezi na kushirikiana na  timu mbalimbali licha ya mahaba yake ya kuipenda Yanga kwani hivi karibuni aliwachangia fedha tawi la Simba walipokuwa wanajiandaa na tamasha  la Simba Day na amekuwa mlezi wa matawi yao sehemu mbalimbali alizofanya kazi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti