• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AFANYA ZIARA STENDI YA MABASI NYEGEZI, ATOA MAAGIZO

Posted on: April 9th, 2025

RC MTANDA AFANYA ZIARA STENDI YA MABASI NYEGEZI, ATOA MAAGIZO


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda leo Aprili 9, 2025 amefanya ziara fupi kwenye stendi ya mabasi  Nyegezi na kutoa maagizo kadhaa yakiwemo mabasi yote kushusha na kupakia abiria ndani ya stendi hiyo.

Akizungumza na Maafisa usafirishaji na watoa huduma mbalimbali ndani ya stendi hiyo iliyopo wilayani Nyamagana, Mkuu huyo wa mkoa amesema hakuna sababu ya wadau hao wa usafirishaji kufungua stendi zisizo rasmi wakati  tayari Serikali imejenga miundombinu ya kisasa.

"Serikali imetumia zaidi ya Tshs bilioni 18 kwa ajili ya kujenga stendi hii ya kisasa ili wananchi wapate huduma bora, sasa kuwepo na stendi zisizo rasmi huko pembezoni kunaszbabisha Serikali kukosa mapato", Mhe. Mtanda.

Amebainisha Ofisi yake ipo mbioni kukutana na wadau hao wa usafirishaji sm pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuweka mkakati imara ya uboreshaji wa huduma ndani ya stendi hiyo.

Aidha Mhe.Mtanda ametoa maagizo kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambao ni wamiliki wa kitega uchumi hicho kurekebisha kasoro zote ambazo ni kero kwa watoa huduma ndani ya stendi hiyo ukiwemo ushuru wa holela,ubovu wa barabara za kuingia stendi na ukosefu wa maji ya uhakika.

"Nimesikia malalamiko kutoka kwa maafisa usafirishaji,wananchi na watoa huduma,nakuagiza meneja wa stendi hii rekebisha kasoro hizo haraka iwezekanavyo tofauti na hapo nikirejea tena hapa na kusikia malalamiko yaliyojirudia nitakuwajibisha",amesisitiza mkuu huyo wa Mkoa.

Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi ambacho kimeishia hatua ya boma,Mtanda ameutaka uongozi wa Jiji kukutana na wadau ili kukusanya nguvu ya pamoja kwa lengo la kukikamilsha na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti