RC MTANDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA MJI WA TULSA- MAREKANI
RC MTANDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA MJI WA TULSA- MAREKANI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Mei 29, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Mji wa Tulsa nchulini Marekani Bw. George Bynum na kuahidiana kuendeleza mahusiano baina ya Jiji la Mwanza na Tulsa.

Akizungumza na ujumbe ulioambatana na Meya huyo kwenye ukumbi Mdogo wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mhe. Mtanda amebainisha kuwa Mwanza ina fursa nyingi za uwekezaji ukiwemo Utalii.




Naye Meya Bynum amesema uhusiano baina ya Majiji hayo umelenga sekta za Elimu, Afya, Utalii na Uwekezaji.