RC MTANDA AMPOKEA KATIBU MKUU WA FRELIMO COMRADE CHAPO AKIWA NJIANI KUELEKEA MARA
RC MTANDA AMPOKEA KATIBU MKUU WA FRELIMO COMRADE CHAPO AKIWA NJIANI KUELEKEA MARA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni12, 2024 amempokea Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO na Mgombea Urais kutoka Msumbiji Comrade Daniel Chapo aliyewasili Mkoani Mwanza akiwa safarini kuelekea Mkoani Mara Wilaya ya Butiama kwa lengo la kuzuru Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere.

Mhe. Daniel F. Chapo amewasili Mwanza akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Comrade John Mongella.

Aidha, mapokezi ya kiongozi huyo yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali waandamizi wa chama na Serikali.

