• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AONGOZA MAPOKEZI YA WAZIRI WA FEDHA JIJINI MWANZA

Posted on: September 17th, 2024

RC MTANDA AONGOZA MAPOKEZI YA WAZIRI WA FEDHA JIJINI MWANZA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewaogoza Wakuu wa Idara, Sehemu na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika mapokezi ya Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba aliyewasili Jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi.

Akizungumza mara baada ya kumpokea Waziri huyo Mhe. Mtanda ameshukuru Mhe. Rais kupitia Wizara hiyo kwakuwa amekuwa akiidhinisha fedha nyingi za miradi mbalimbali inayotekelezwa Mkoani humo ikiwemo ile ya kimkakati kupitia Wizara ya Fedha.

"Ofisi yangu imekuwa ikipokea fedha nyingi sana, kipekee ninamshukuru sana Mhe. Rais ameendelea kutuletea fedha nyingi za miradi kupitia wizara yako, na sisi tunakuahidi Mhe. Waziri tutaendelea kuzisimamia fedha hizi ili zikatumike kama ilivyokusudiwa kwa lengo la kuwaletea wananchi wa Mwanza maendeleo". Amesema RC Mtanda.

Naye Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema ujio wake katika Mkoa wa Mwanza ni kuja kukagua, kuzindua na kutembelea miradi mbalimbali ambayo Serikali imekuwa ikiitekeleza katika Mkoa wa Mwanza na kuzungumza pia na wananchi kuwaleza namna serikali inavyoeendelea kuratibu na kutekeleza miradi hiyo.

Mhe. Dkt. Mwigulu amesema Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa akitoa fedha nyingi za miradi na ameendelea kukuhakikisha anatimiza ahadi yake ya kuwaletea maendelea wananchi wa Tanzania hivyo amedhamiria kutembelea na kukagua miradi yote kuanzia ngazi za juu mpaka za vitongoji ili kujionea ufanisi wa utekelezaji wa miradi hiyo.

"Nimeambatana pia na Wataalamu wangu kutoka Wizarani lakini pia kutoka maeneo mbalimbali ya kisekta ili kuhakikisha katika ziara hii pia tunatatua na kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo yale ya kimfumo kama vile NeST". Amesema Waziri wa Fedha.

Mhe. Dkt. Mwigulu aliwasili Mkoani Mwanza ijumaa ya tarehe 13 Septemba 2024 ambapo alianza ziara yake rasmi Wilayani Misungwi kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Mwanza na kisha kuzungumza na Wananchi wa Misugwi Mjini na leo ameendelea na ziara yake Wilayani Nyamagana ambapo atakagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Mjini Kati Jijini Mwanza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti