• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATAKA KANUNI ZA KILIMO BORA ZAO LA PAMBA ILI KUONGEZA UZALISHAJI

Posted on: November 18th, 2024

RC MTANDA ATAKA KANUNI ZA KILIMO BORA ZAO LA PAMBA ILI KUONGEZA UZALISHAJI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wakulima wa pamba mkoani humo kung'oa na kuchoma moto mazalia ya Pamba ya msimu uliopita kabla ya Septemba 15 ya kila mwaka ili kutoathiri msimu mpya wa kilimo hicho.

Mhe. Mtanda ametoa agizo hilo mapema leo Jumatat  Novemba 18, 2024 wakati akifunga kikao cha viongozi ngazi ya wilaya kwa ajili ya kampeni ya ung'oaji wa masalia ya Pamba wilayani Kwimba.

Amesema kutofanya hivyo kunasababisha wadudu kuzaliana na kusubiri pamba mpya shambani kuiharibu, hivyo ili kujihakikishia uzalishaji wenye tija ni lazima wakulima wafuate kanuni za kilimo cha zao hilo kwa kusafisha mashamba mapema kabla ya msimu mwingine.

"Viongozi wote mpo hapa maafisa ugani, tarafa, kata na vijiji nawaagiza  muda wa hiyari umekwisha twendeni tukatekelze kanuni bora za kilimo cha Pamba kwani zao hili ndio injini ya uchumi wa wananchi wa Mwanza kwa miaka mingi." Mtanda.

Aidha, ameipongeza bodi na kwa kipekee balozi wa Pamba nchini,Aggrey Mwanri kwa juhudi zake za uelimishaji wakulima wa Pamba nchini na kwa kipekee mkoani Mwanza ambako kimsingi amechagiza uzalishaji na kufanya idadi ya wakulima waliopo mkoani humo kuwa sawa na waliopo kwenye mikoa 17 nchini.

Balozi wa Pamba Mhe. Agrey Mwanri amesema tatizo kubwa linalokwamisha Mbegu mpya kumea kwenye mashamba ya Pamba ni wakulima kutong'oa maotea ya pamba ya msimu uliopita kwani msimu mpya unachelewa na hatimaye mvua za vuli zinawapita.

Amefafanua kuwa mwisho wa kusafisha pamba ni tarehe 15 Septemba, 2024 ya kila mwaka ili msimu mpya uanze lakini wapo baadhi ya wakulima wamekua wakiacha maotea kwa lengo la kulisha mifugo kinyume na kanuni za kilimo bora na kupelekea kukwamisha uzalishaji.

"Mkiruhusu mimea ya msimu uliopita kuendelea kubaki shambani mtakua mnakaribisha wadudu kama Chawajani, Kandambili na ndio maana hivi sasa neema na baraka ya zao la pamba kwenye uchumi wa wananchi zimepungua kutokana na kushuka kwa takwimu za uzalishaji."  Mwanri.

Aidha, amekemea tabia ya wakulima kuchanganya mazao na akatoa mfano wa Pamba na Mahindi yakioteshwa kwenye shamba moja yanasababisha zao moja kushiba rutuba na kulikwamisha jingine na kwakua Mahindi yanamea kwa haraka basi pamba itaathirika.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti