• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATOA POLE, AHIMIZA UCHUNGUZI JANGA LA MOTO SABASABA KUKAMILIKA HARAKA

Posted on: March 17th, 2025

RC MTANDA ATOA POLE, AHIMIZA UCHUNGUZI JANGA LA MOTO SABASABA KUKAMILIKA HARAKA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda leo Machi 17,2025 amewatembelea wafanyabiashara wa mbao eneo la Sabasaba wilayani Ilemela waliopatwa na ajali ya moto na kuwapa pole na kuwaomba kuwa na utulivu wakati  taarifa ya uchunguzi wa chanzo cha moto huo ikiendelea kufanyika.

Akizungumza nao mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na moto huo,mkuu huyo wa mkoa amesema mara baada ya taarifa hiyo kukamilika na kusomwa, Ofisi yake itakutana na wafanyabiashara hao pamoja na taasisi za fedha ili kuona namna ya kuwapa muda zaidi wa marejesho ya fedha kwa wale waliokopa.

"Natoa rai kwa vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi huu ili kutambua chanzo na kujua nini kifanyike na wafanyabiashara hao waendelee na shughuli zao mapema iwezekanavyo kama Serikali inavyohimiza wananchi kuwajibika",Mtanda

Aidha amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia matumizi ya vifaa vya kuzimia moto na bima ambayo itawasaidia kuepuka hasara kubwa yanapotokea majanga ya moto kama hilo.

Amebainisha mara baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika na moto huo amepata taarifa idadi kubwa hawatumii vifaa vya kuzimia moto licha ya elimu ya matumizi hayo kutolewa mara kwa mara na Jeshi la zimamoto na uokoaji.

"Serikali kuna maeneo ya majanga inawajibika moja kwa moja kuwagharamia wananchi na mengine haiwajibiki nayo kama hili,narudia kuwakumbusha kuzingatia sheria zinavyotaka ili kujihakikishia usalama wa muda wote wa mali zenu,niwapongeze pia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufanya kazi hii kwa weledi na kuokoa sehemu kubwa ya mali za wafanyabiashara hawa,"mkuu wa mkoa

Kwa upande wake kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza SSF Elisa Kamugisha amebainisha moto huo ulianza majira ya saa saba usiku na kufanikiwa kwa asilimia kubwa kuwahi kuuzima usienee sehemu nyingine.

"Hapa kuna wafanyabiashara wa mbao zaidi ya elfu moja lakini walioathirika na janga la moto ni thelasini,lakini taarifa rasmi itatolewa muda siyo mrefu"SSF Kamugisha.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti