• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA ATOA WITO KWA COPRA KULETA MAGEUZI CHANYA MAZAO MCHANGANYIKO

Posted on: January 8th, 2025

RC MTANDA ATOA WITO KWA COPRA KULETA MAGEUZI CHANYA MAZAO MCHANGANYIKO


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Januari 8, 2025 amefanya mazungumzo ofisini kwake na uongozi kutoka Mamlaka ya udhibiti wa nafaka na mazao mchanganyiko (COPRA) na amewataka kuleta mageuzi chanya kwenye mazao inayosimamia.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo mpya iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo, bi. Irine Mlola katika mazungumzo na mwenyeji wao umeombwa kuhakikisha inawaleta wataalamu bora ambao wataongeza tija ya mazao yaliyokusudiwa ambayo ni nafaka na jamii ya mikunde.

"Hongereni kwa kuja na mpango huu mzuri maana tangu miaka ya nyuma tulikuwa tunasikia mazao ya biashara na chakula, lakini ukweli ni kwamba sasa kilimo chote ni biashara hayo mazao yaliyokosa usimamizi naamini yataingia kwenye mnyororo wa thamani," RC Mtanda.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameihakikishia Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Ofisi yake kuwakusanya wadau wa mazao ya nafaka na mikunde ili kuwajengea uelewa wa taasisi hiyo na makusudi yake kwenye kilimo hicho kwa ujumla.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa lengo la ujio wetu kwanza ni kujitambulisha na kukufahamisha majukumu ya taasisi hii ambayo ilianzishwa mwaka 2023 na kuanza rasmi kazi mwaka jana, kusimamia shughuli za masoko kwa mfumo wa stakabadhi gharani kwa mazao 5-6 yakiwemo Kokoa, Ufuta, Soya, Mbaazi, Dengu na mwaka huu 2025 tumeongeza zao la Choroko", Irine Mlola, Mkurugenzi COPRA.

Uongozi huo umepita mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kwa lengo la kuitambulisha Taasisi hiyo na kufungua Ofisi zao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti