• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AWAHIMIZA VIJANA UMUHIMU WA KUCHAPA KAZI KATIKA KUJILETEA MAFANIKIO

Posted on: June 15th, 2024

RC MTANDA AWAHIMIZA VIJANA UMUHIMU WA KUCHAPA KAZI KATIKA KUJILETEA MAFANIKIO


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka vijana Mkoani humo kuhakikisha wanafanya kazi kwa hali na mali ili waweze kufikia malengo na mafanikio waliyo jiwekea.

Akiongea leo Juni 15, 2024 wakati alipotembelea shindano la kusaka mzalendo namba moja kwa nchi yake mwenye kujua Rais Samia amefanya nini katika Mkoa wa Mwanza (Samia Challenge)  Mtanda amesema haamini katika njia nyepesi ya mafanikio, hata  ukuu wa Mkoa, siamini kutumia ukuu wangu wa Mkoa kuniondolea umaskini wangu.

"Kwa hiyo ukitaka njia rahisi kupitia ukuu wa Mkoa basi utataka kula rushwa utawaonea watu ili upate pesa ununue ghorofa, ununue gari zuri uwe na maisha mazuri mwisho wa siku hata safari hii ya ukuu wa Mkoa itakuwa safari fupi." Amesema RC Mtanda.

Aidhe, Mhe. Mtanda amewataka Vijana hao kukaa mbali na tamaa kwani sio kila kitu wanavyo vitamani wanaweza kuvipata, hali inayoweza kuwapelekea kuishia pabaya na wakashindwa kufikia mafanikio na malengo waliyojiwekea kwa sababu ya tamaa.

Akiongelea maadili, Mhe  Mtanda amewataka vijana wa kike kutokubali kutumika vibaya au kununulika kwa kuelewa na kutambua thamani yao, kwa kuweka jitihada katika mambo wanayoyafanya na Mungu atawasaidia kwa sababu kwenye nia pana njia.

"Katika jambo ambalo nikikutana na  Vijana napenda kuwausia ni umuhimu wa kujali na kutunza afya zao, hakuna maendeleo wala mafanikio bila ya afya bora, huwezi kutimiza ndoto zako za maisha kama afya haiko sawa sawa, lakini pia afya ikishayumba utatumia fedha na muda mwingi katika kushughulikia afya zetu. Ameongeza Mhe. Mtanda.

Mtanda kadhalika amewataka Vijana hao kuhakikisha wanatenga muda wa kufanya mazoezi na kujiepusha na vitu vinavyoweza kuharibu afya ikiwemo uvutaji wa sigara, bangi, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya, ngono zembe na vitu vyote vinavyochochea uharibifu wa afya.

Akihitimisha hotuba yake Mkuu huyo wa Mkoa amewapongeza vijana hao kwa ushiriki wao, aidha amesema hapa Mwanza Serikali ya Rais Samia ipo imara chini ya uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa na amewataka vijana hao pia kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita kwa kufanya kazi kwa bidii.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti