• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AWATAKA WANUFAIKA WA MRADI WA VIZIMBA KUWEKA UMAKINI KATIKA UWEKEZAJI HUO

Posted on: August 7th, 2024

RC MTANDA AWATAKA WANUFAIKA WA MRADI WA VIZIMBA  KUWEKA UMAKINI KATIKA UWEKEZAJI HUO


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka vijana waliokopeshwa vizimba vya kufugia samaki Kanda ya Ziwa Viktoria hususani Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanaweka umakini wa kutosha katika usimamizi wa uwekezaji huo ili uwaletee manufaa.

Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Agosti 07, 2024 alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo  uliotolewa kwa mkopo bila riba kupitia benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) kwa makundi maalum ya wanawake, walemavu na Vijana katika mtaa wa Kisoko uliopo Wilayani Nyamagana.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wanufaika hao kuzingatia pia utunzanji wa kumbukumbu kwa kipindi chote wawapo shambani hapo, aidha ameutaka uongozi wa mahali hapo kuhakikisha wanakuwa na daftari maalumu la wageni ambalo pia watalitumia kuandika maoni yao ili wakija viongozi na wageni mbalimbali watumie daftari hilo katika kutazama na kuona ni kwa namna gani wanaweza wakatatua changamoto au kero zilizoainishwa katika daftari hilo.


"Mali bila daftari huisha bila habari,  ni lazima muwe na daftari la wageni hata kama anakuja DC anakuta mmendika changamoto ya barabara basi yeye atajua ni namna gani ataliwasilisha suala hilo kwa mamlaka husika na changamoto yenu inakua imepata tiba". Mhe. Mtanda.

Kadhalika Mhe. Mtanda amewataka wanufaika hao kuweka umakini wa hali ya juu kwa kuwa na usimamizi bora wa vizimba hivyo kwa kuwa Serikali ya Rais Samia imedhamiria kwa dhati kuwasaidia wananchi wake kujikwamua na umaskini kwa kuwapatia wanufaika hao zaidi ya shilingi bilioni 4 katika uwekezaji huo wa ufugaji wa samaki wa vizimba.

"Msifanye mambo kwa kutania tania, kama mmedhamiria kufanya uwekezaji hapa ziwani basi acheni ubabaishaji kuweni makini katika kusimamia, msipofanya hivyo nyie wapo wageni watakaokuja kuitumia fursa hii vizuri. Ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Mkoa wa Mwanza umebahatika kupata wanufaika wengi ambao ni 69 (Vikundi, ushirika  na watu binafsi wenye wanufaika 1305) pamoja na vizimba 255 vya mkopo usio na riba, ambapo kwa eneo la Kisoko pekee vimesanikishwa vizimba 112 na kuna jumla wanufaika 392 kwa awamu ya kwanza na ya pili.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti