• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC MTANDA AZUNGUMZA NA WAZEE WA KWIMBA AWAAHIDI KUMALIZA KERO ZA MAJI NA BARABARA

Posted on: June 6th, 2024

RC MTANDA AZUNGUMZA NA WAZEE WA KWIMBA AWAAHIDI KUMALIZA KERO ZA MAJI NA BARABARA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amesema Serikali ipo mbioni kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa Ngudu na wote wilayani Kwimba kwa kujenga mradi mkubwa pamoja na kuharakisha uwekaji Lami kwa kilomita 3 za mjini na baadae kupeleka hadi Mabuki.

Mhe. Mtanda ametoa ahadi hiyo leo Juni 06, 2024 wakati akizungumza na Wazee wa Kwimba katika kikao chake kifupi alichoketi nao kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.


"Leo nimefanya kazi kama ya Tomaso maana nimeona na kuamini kuwa Ngudu na Kwimba kwa ujumla wanapata adha ya barabara na nawaahidi tutaanza kujenga hizo Kilomita 3 za hapa na baadae tutatafuta fedha ili kuunganisha Kilomita zote 26 hadi barabara kuu kule Mabuki", amesema Mhe. Mtanda.

Aidha, ametoa wito kwa vituo vya afya, zahanati na Hospitali ndani ya Wilaya hiyo na zingine kuhakikisha wanatoa upendeleo kwa wazee kwa kuimarisha  madirisha ya kuhudumia wazee wanapofika kwenye vituo hivyo kupata huduma za afya.


"Watoto wa kike wapewe fursa ya kusoma, ni uwekezaji mkubwa kuliko kupokea ng'ombe wa mahari, tuwaache wasome ili baadae wawe madaktari wazuri na waweze watusaidie" amesisitiza Mkuu wa Mkoa.


Naye, Mzee Edward Seneda Mwenyekiti wa Wazee Kwimba amezungumzia furaha yake kwa kupata fursa ya kuzungumza na  Mkuu wa Mkoa na kueleza changamoto zao na kuzichukua kwa ajili ya kuzifanyia kazi siku za usoni.

Shekhe wa Wilaya na Kiongozi wa Kamati ya Amani na Kiongozi wa Sungusungu wametumia wasaa huo kushukuru Serikali ya wilaya kwa kuwajali na kushirikiana nao kwenye shughuli mbalimbali na wamemtakia Mkuu wa Mkoa kheri katika shughuli zao.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti