• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC-MWANZA Azindua Chanjo ya Matone ya Polio Ukerewe

Posted on: May 18th, 2022

Mkoa wa Mwanza umepanga kuhakikisha inatoa chanjo kwa watoto 846,733 na imejipanga katika vituo 355 ambapo jumla ya watoa huduma 6,909 wamepata mafunzo kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel leo Mei 18,2022 alipokuwa akizindua  Chanjo ya matone ya Polio katika kituo cha Afya Nakatunguru kilichopo Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

 "Ukerewe ina jumla ya wakazi 518,114 kati yao watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 ni 108,937 ambao ndiyo lengo la chanjo ya Matone ya Polio," amesema Mhandisi Robert Gabriel.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema,tulizoea kufanya shughuli hizi za uzinduzi makao makuu ya Mkoa na kuahidi kuwa  ni mwanzo wa kufanya Shughuli za kimkoa na nyingine zitaendelea kufanyika Wilayani hapa.

"Kampeni hii itafanyika kwa siku 4 kuanzia tarehe 18 hadi 21 Mei 2022 ambapo lengo ni kuchanja watoto 846,733 katika Mkoa Mzima kwa Wilaya ya Ukerewe inatakiwa kuchanja watoto 108,937."

Dkt.Rutachunzibwa ameongeza kuwa Chanjo zitatolewa kupitia vituo 355 vikiwemo vituo 38 vya Wilaya ya Ukerewe na Watoa huduma 6,909 wamepata mafunzo kwa ajili ya kazi ya Uchanjaji,Watunza takwimu na wahamasishaji.

"Tumesambaza chanjo Dozi 973,740 katika vituo vyote na maandalizi ya kutoa chanjo hiyo yamekamilika na chanjo hii inatolewa bila malipo.

Naye Diwani wa kata ya Nakatunguru,Mataba Sosthenes ameshukuru kwa uzinduzi wa kampeni ya Polio katika kata yao na  amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel kuwasadia katika maboresho ya huduma mbalimbali katika kituo cha afya cha Nakatunguru.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti