• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC - Mwanza azindua wiki ya Huduma za Maabara Uwanja wa Furahisha

Posted on: May 2nd, 2022

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, amewaagiza wanasayansi wa Maabara za afya mkoani humo kuongeza usimamizi wa ubora wa vipimo mbalimbali katika maabara zote za serikali na binafsi  ili kujihakikishia huduma bora.

Mhe. Mhandisi Gabriel pia amewataka wataalamu hao kuongeza kasi ya ukusanyaji wa damu kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya damu kwa wahitaji wote.

Mhandisi Gabriel ametoa maagizo hayo leo Mai, 2 wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya wataalamu wa maabara za afya kimkoa yanayofanyika uwanja wa furahisha hadi Mei , 6 mwaka huu kwa uratibu wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya (MeLSAT)mkoani humo.

"Niwatake  wataalamu wa afya mfanye kazi kama timu  na kutumia majibu ya maabara (takwimu), muweke mipango endelevu itakayowasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbal,"amesema na kuongeza

"Ukusanyaji wa damu umeendelea kufanyika kwa mafanikio  ya kiasi cha kufikia asilimia 69 ya malengo ya kukusanya  chupa za damu 32,173 kwa mwaka.

Naye Makamu wa Rais MeLSAT, Taifa, Joseph Gimbuya, amesema  ili kuboresha afya za watanzania mkazo wa kwanza uwe katika kinga na wa pili katika tiba.

"Lakini tiba isiyo  na uchunguzi sahihi wa kiini na aina ya ugonjwa ni kazi bure  na huongeza gharama kwa mgonjwa, serikali na taifa kwa ujumla.

" Hivyo tunapotafakari matibabu  sahihi yenye gharama nafuu zaidi, matumizi ya maabara ni lazima kwa tabibu ama daktari maana kufanya kazi bila maabara ni sawa na kupiga Ramli au kuwa mganga wa kienyeji,"amesema Gimbuya.

Naye Mwenyekiti wa MeLSAT Mkoa wa Mwanza,  Betrand Msemwa, amesema wanachama wote  wana ari ya kuwahudumia wananchi wakishirikiana na wanataaluma wengine ili kuhakikisha afya za wananchi zinazidi kuwa bora.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa, ametoa wito kwa wataalamu wa maabara kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kuwataka washirikiane ili kulinda taaluma hiyo ili  isichafuliwe na watu wachache wenye nia ovu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti