• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RC Mwanza azitaka Halmashauri kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha

Posted on: June 28th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, ametoa siku 90  kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe kuwatafuta watumishi 53 ambao wamelipwa mishahara Jumla ya Tshs Milioni 486 kwa mwaka wa fedha 2015/16 wakati wakiwa wameshastaafu.

Mhandisi Gabriel ametoa agizo hilo leo Juni 28, 2022 baada ya kuibuka hoja katika kikao Maalum cha Madiwani cha kujadili Utekelezaji wa Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambapo Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo Mang'oha Maginga alisema awali walikuwa wanadai Tshs milioni 657 kwa watumishi waliolipwa fedha wakiwa wamestaafu na wengine wakiwa wamefariki.

Ndugu Maginga aliendelea kufafanua kwamba baada ya kufuatilia kwa kina watumishi 21 walirejesha Tshs Milioni 111.1 hivyo deni lililobaki ni Tshs Milioni 486 ambazo wanadaiwa watumishi 53 ambao wako hai huku watumishi 21 waliofariki dunia wakiacha deni la shilingi milioni 63.

"Hawa watu wapo katika mfumo wa malipo ya mifuko ya hifadhi ya jamii na wana namba za hundi za malipo hivyo kutokuwafualia kwa kipindi chote hicho ni uzembe wa hali ya juu yaani haiingii akilini mnakuja kuwabaini leo kwenye kikao, sasa nahitaji ndani ya siku 90 fedha hizo za Umma zirudi." Mhandisi Gabriel.

Baada ya kuibuka hoja ya kudaiwa zaidi ya Tshs Bilioni 1 zilizokopwa kutoka kwenye Akaunti ya Amana, Mhe Mkuu wa Mkoa amewaagiza Halmashauri hiyo kuacha tabia ya kukopa fedha na badala yake amewataka kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kujiendesha kutokana na Mapato ya Ndani.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mwanza, Waziri Shabani amefafanua kuwa kwa hesabu za mwaka wa Fedha 2020/21 Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe imepata Hati Inayoridhisha.

Mkutano Maalumu wa  kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG katika halmashauri ya wilaya Ukerewe umehitimisha ziara ya Mhandisi Gabriel ya kujadili hoja katika Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza zilizoanza juni 20 mwaka huu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti