• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

RMO MWANZA APOKEA TELEVISHENI 57, KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA KWENYE VITUO VYA AFYA

Posted on: February 7th, 2024

RMO MWANZA APOKEA TELEVISHENI 57, KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA KWENYE VITUO VYA AFYA


Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa amepokea Televisheni 57 Kutoka Wizara ya afya kwa lengo la kutoa taarifa na kusaidia utoaji wa huduma bora kwenye vituo vya afya mkoani humo.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Februari 07, 2024 kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa ukiwakutanisha Wawakilishi kutoka Wizara hiyo, TAMISEMI na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

"Tunategemea kuwa hizi televisheni zitaeneza ujumbe ambazo wagonjwa pamoja na watumiaji wa vituo vyetu watakuwa wanavifuatilia wakipata mafunzo mbalimbali kutoka kwenye mada mbalimbali ambazo zinahusiana na masuala ya afya" Mganga Mkuu.

Dkt. Rutachunzibwa ametumia wasaa huo kuwataka wananchi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari za kuepukana na Ugonjwa hatari wa Kipindupindu.

Mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Jaina Msuya amesema lengo la Mradi huo ni kupeleka umeme kwenye vituo vya afya na pampu za maji vijijini ambao unafikia vituo vya afya 57 nchi mzima pamoja na pampu za maji 363 ambazo zimesambaa kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa gharama ya mradi ni billion 37.4.

"Lengo la kuanzisha huu mradi ni kuwawezesha wananchi wanaokaa maeneo ya vijijini waweze kupata huduma kwa haraka na muda sahihi." Amefafanua.

Pia amewataka wananchi kutumia maji ambayo ni safi na salama yawasaidie katika matumizi yao ya kila siku kwa sababu yatawasaidia kuwalinda na kutunza afya zao,  na itapunguza  kero ya kutafuta maji kwa umbali mrefu hasa kina mama na kuweza kupata muda wa kushiriki kwenye majukumuu mengine kama ya kifamilia.

Mwakilishii kutoka Wizara ya afya James Mhilu ameishukuru wakala wa nishati vijijini (REA) pia ameongeza kwa kuelezea  namna gani mradi huo unaenda kuwasaidia wananchi moja kwa moja, uhakika wa maji na vituo vya kutolea huduma za afya  kupata umeme na kuhakikisha kuwa huduma ya chanzo itaimarika ili kuweza kupambana na magojwa ya mlipuko kama kipindupindu na kuwataka watu wazingatie unawaji wa mikono kwa maji safi na sabuni ili kuepukana na magonjwa, lakini pia mradi huu unaenda kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika vituo vya afya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti