• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

SEKTA YA MADINI INAENDELEA KUKUA KWA KASI NCHINI : WAZIRI MAVUNDE

Posted on: January 5th, 2024

SEKTA YA MADINI INAENDELEA KUKUA KWA KASI NCHINI : WAZIRI MAVUNDE


Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema Sekta hiyo inazidi kukua ambapo 2022/23 Mauzo ya bidhaa za Madini nje ya nchi yalifikia 56% huku Mzunguko wa fedha ukichangia zaidi ya Trilioni 1.6 na zaidi ya Bilioni 678 zikikusanywa kama Maduhuli ya serikali zinazotokana na vyanzo mbalimbali vya mapato kwa zaidi ya Trilioni 2 ambayo ni 15% ya pato lote.

Mhe. Mavunde amebainisha hayo  mapema leo tarehe 05 Januari, 2024 kwenye Ukumbi wa Rock City Mkoani Mwanza wakati akizungumza na watoa huduma kwa wamiliki wa Leseni za Madini kwenye Mkutano uliowakutanisha wadau ili kujadili namna bora ya kuboresha sekta hiyo ili washiriki kwenye Uchimbaji waongezeke.

"Hadi sasa tumefanya utafiti kwa 16%  na lengo letu kubwa ni kubaini madini tuliyonayo na kuweza kujipanga ili kusaidia wananchi kuacha kufanya uchimbaji kwa kuhisi na hadi kufikia 2030 wananchi watakua wanajua hapa kuna nini kwa taarifa sahihi kutoka wizara ya Madini." Waziri Mavunde.

Vilevile, amebainisha kuwa wizara ya Madini ipo tayari kufanya maboresho ya kisheria ili kutoa fursa zaidi kwa washiriki kuweza kujihusisha na uchimbaji wa Madini nchini huku akitoa wito kwa taasisi za kifedha kuendelea kuwezesha mitaji ili watanzania wengi washiriki kwenye kuchimba na kuchangia rasilimali kwenye utoaji huduma kigodini.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ameipongeza Wizara ya Madini kwa kufanya Utafiti wa kubaini ni eneo gani lina Madini ya aina gani na kwa kiasi gani kwani litasaidia kupunguza gharama za uendeshaji kwenye sekta hiyo nchini.

"Hakika Waziri Mavunde unafanya kazi nzuri kwa manufaa ya watanzania, ulipokua Naibu kwenye Kilimo ulifanya tafiti kuhusiana na Afya ya Udongo na huku kwenye Madini umekujq na jambo zuri la kubaini ni wapi kuna madini, ya aina gani na kwa kiasi gani, hapa utasaidia." Makalla.

Aidha, Mhe. Makalla amebainisha kuwa uwanja wa ndege wa Mwanza upo kwenye maboresho makubwa kuanza kuhudumia wasafiri na wasafurishaji wa Mizigo hivyo wadau wa sekta ya Madini watapata fursa ya kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi kwa ufanisi.

"Kutakua na Mgodi Mkubwa wa Madini ya Dhahabu wilayani Sengerema (Nyanzaga) ambao utashika nafasi ya Pili nchini ambao upo kwenye hatua mwisho kuanza kazi, nawaomba wanaMwanza mjiandae kunufaika na fursa." Makalla.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti