• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI NA ITAENDELEA KUWABORESHEA MIUNDOMBINU: RC MTANDA

Posted on: May 13th, 2024

SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI NA ITAENDELEA KUWABORESHEA MIUNDOMBINU: RC MTANDA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda ameendelea na kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kutambuana ambapo leo Mei 13,2024 amekutana na Maafisa Usafirishaji maarufu kama bodaboda kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela na kuwaambia Serikali inatambua mchango wa Sekta binafsi na inaendelea kuwawekea mazingira mazuri ya miundombinu ili wafanye kazi zao vizuri.

Akizungumza na Maafisa hao eneo la Buhongwa Wilayani Nyamagana, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Sekta binafsi na rasmi zote zinachangia pato la taifa hivyo Serikali imekuwa na wajibu wa kuhakikisha wanafanya kazi zao katika mazingira rafiki huku wakifuata miongozo yote ya sheria za nchi.

"Ndugu zangu Maafisa Usafirishaji nimewafuata hapa leo lengo  ni kutambuana nina karibu mwezi sasa tangu nihamishiwe hapa,rai yangu kwenu kuweni mabalozi wazuri wa amani na kuzingatia sheria zote za barabarani ili kuepusha ajali,kero zenu nazitambua nawahakikishieni zitapatiwa ufumbuzi," Mkuu wa Mkoa.

Mtanda amebainisha Maafisa Usafirishaji hao wanafanya shughuli zao ili kuhudumia familia zao na siyo vinginevyo, hivyo hayuko tayari kusikia kuna aina yoyote ya uonevu dhidi yao au kuwakwamisha kutekeleza majukumu yao, amewahakikishia pia kuwawekea mazingira mazuri ya kukopeshwa.

Aidha amewataka Maafisa hao kufanya kazi kwa kuzingatia miiko ya kazi zao na Serikali haitakuwa tayari kuwaona baadhi yao wakijihusisha na uvunjifu wa amani.

"Mhe.Mkuu wa Mkoa barabara ya Sawa haipitiki tunaomba sana tusaidie ifanyiwe marekebisho maana vyombo vyetu vinachakaa kwa haraka kutokana na hali hiyo," Bosco Yohane,Afisa usafirishaji

Akiwa Wilayani Ilemela na Maafisa Usafirishaji wa pikipiki za miguu mitatu (Bajaii) amesema anatambua mvutano uliopo baina ya Bajaj na daladala na  maeneo ambayo hawaruhusiwi kuingia na amewahakikishia changamoto hiyo itapatiwa ufumbuzi akishirikiana na wakuu wa Wilaya na sekta nyingine kama LATRA, TARURA na Taasisi za Bima.

"Ndugu zangu katika mkutano huu sina mengi zaidi ya kufahamiana ili mkaendelee na shughuli zenu, nawahakikishieni ushirikiano kati ya Serikali nanyi zingatieni amani na usalama na epukeni kutumika vibaya muwe wa kwanza kuwadhibiti wenzenu ambao mtaona wanakwenda kinyume na Sheria za nchi," Mkuu huyo wa Mkoa.

Mhe. Mtanda amesema Mwanza imeingiziwa Shilingi Bilioni 1.2 za mikopo kwa yale makundi maalum wakiwemo vijana, utaratibu utafanyika ili waweze kunufaika na amepongeza pia Afisa Usafirishaji kutoka Jeshi la Polisi (RTO) Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sunday Ibrahimu na kumtaka kuongeza bidii ili Maafisa Usafirishaji hao wafanye kazi zao vizuri bila bugudha.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti