• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali Yajipanga kuboresha huduma za Meli

Posted on: June 21st, 2019


Serikali imetenga Sh bilioni 5.9 katika mwaka huu wa fedha ambazo zitatumika katika kuajiri ajira mpya, kulipa mishahara ya watumishi sanjari na uboreshaji wa shughuli za Kampuni ya Huduma za Meli Nchini ( MSCL).

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini hapa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele wakati wa ziara yake ya kikazi ambapo alipata fursa ya  kutembelea ujenzi wa mradi wa chelezo, eneo ambalo litatumika kuunda meli mpya iliyoahidiwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa na kukagua ukarabati unaoendelea  wa meli za MV Victoria na MV Butiama.

Alisema lengo la serikali kutoa kiasi hicho cha fedha ni kuiwezesha Kampuni hiyo ya huduma za meli ya serikali kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma za usafirishaji wa majini  sayansi na pia kuondokana na changamoto za muda mrefu ambazo zilikuwa ni kikwazo katika kipindi cha miezi 27 ili baadaye iweze kujitegemea na kutoa gawio la fedha serikalini.

Alisema kabla ya kutoa fedha hizo, tayari serikali kupitia kwa Rais Dk. John Magufuli alitoa kiasi cha Sh bilioni 2.1 kwa ajili ya kuwalipa watumishi waliokuwa wamekaa muda mrefu bila ya kulipwa mishahara yao na kuifanya MSCL kuendelea kuwa chombo imara zaidi katika utekelezaji wa majukumu yake.


“ Nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kwamba serikali imeyamaliza matatizo yaliyokuwa yanaikabili MSCL na sasa inakwenda kutekeleza majukumu yake vyema,” alisema.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL  Mhandisi Erick. B. Hamissi alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa fedha ambazo sasa zinaweza kuondoa changamoto ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zinaikabili kampuni ya MSCL.


Alisema Rais John Magufuli ameonyesha kuwa ana nia njema na MSCL na wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuiwezesha MSCL na kuhakikisha huduma za usafiri wa majini zinaaimarika kwa manufaa mapana ya kuimarisha uchumi wa kanda ya ziwa na taifa kwa ujumla.


Alisema kwa muda wowote sasa serikali kupitia MSCL inatarajia kusaini mkataba mwingine wa ujenzi wa meli mpya katika Ziwa Tanganyika itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo , ukarabati wa meli ya Mv Liemba iliyo katika Ziwa Tanganyika na ukarabati wa meli za Mv Umoja na Mv Serengeti ambazo zitakapokamilika zitaanza kufanya shughuli za usafirishaji katika Ziwa Victoria.


Alisema miradi hiyo minne ambayo haijsainiwa, ikiwemo ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli hizo ( MV Liemba, MV Umoja na MV Serengeti-Ziwa Victoria, alisema tayari MSCL imeishamaliza taratibu zote za manunuzi na kuandaliwa mikataba na kwamba taratibu zote za kusainiwa kwa mikataba hiyo zinaendelea kukamilishwa.


Aidha alisema kuwa serikali pia imetenga kiasi cha fedha Sh bilioni 70 katika mwaka ujao wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya za mizigo zinazotarajia kufanya huduma ya usafirishaji katika Ziwa Tanganyika na Victoria ambapo fedha hizo pia zitatumika kwenye ukarabati wa mkubwa wa meli ya Mt Sangara iliyoko Ziwa Tanganyika.

“Kwa sasa hatujapata wakandarasi na kwenye mradi hiyo kwa sasa tuko kwenye hatua ya manunuzi,” alisema Hamissi.


Alisema mikakati ya MSCL ni kutekeleza Rasimu ya Mpango Mkakati wa muda mrefu kuanzia 2019-2025, hii ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya meli za kusafirisha mabehewa ndani ya Ziwa Victoria, kujenga meli kubwa ya kubeba mafuta katika ziwa Tanganyika, kujenga meli kubwa ya kubeba mizigo hususani makontena katika Ziwa Tanganyika na Victoria.


“ Hii ni pamoja na kuhakikisha ukarabati wa meli za MV Victoria na Butiama na ujenzi wa cherezo unakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kuruhusu ujenzi wa meli mpya katika ziwa Victoria ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais kutekelezwa kama ilivyopangwa,” alisema Hamissi.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti