• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali yatenga Shs Bilioni 40 Kwa ajili ya Wataalamu wa Utafiti wa mazao ikiwemo Pamba

Posted on: December 7th, 2022


Serikali katika kuhakikisha inaboresha zao la Pamba na kumuwekea mazingira rafiki Mkulima imeongeza bajeti ya Utafiti kwa Wataalamu wa kilimo kutoka Shs Bilioni 11.7 hadi kufikia bilioni 40 na bajeti ya Mbegu ikitengewa Shs Bilioni 43.

Akizungumza leo wakati wa ugawaji zana za kilimo na usafiri zenye lengo la uboreshaji wa zao la Pamba kwenye   Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI kilichopo Wilayani Misungwi,Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde amesema bajeti hiyo ya utafiti imelenga pia kuboresha Maabara zote za udongo ili kumuhakikishia Mkulima uhakika wa kilimo chake na kupata mazao bora.

Amesema Serikali hii chini ya uongozi wake Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuleta mageuzi ya kweli kwenye Sekta hiyo ikitenga bajeti ya Shs Bilioni 361 ambazo zimelenga kuleta mageuzi chanya sehemu mbalimbali ukiwemo mkakati kamambe wa kuwapa ajira vijana.

"Tumeanza mradi huo kwa Vijana kuwawekea mazingira mwafaka ya kilimo kwa kuanza na Mikoa 2 ya Dodoma sehemu za Chamwino na Mbeya huko Chunya na kutenga jumla ya hekari 69000 lengo likiwa kuwafikia Vijana milioni 3  kabla ya mwaka 2030 wawe na ajira kupitia Sekta hiyo" Mhe.Mavunde

Amewakumbusha Wataalamu wa kilimo kwenye Kituo cha Utafiti Ukiriguru kuongeza ubunifu zaidi ili Mkulima azidi kupata tija kwenye mazao yake hasa Pamba ambayo ndiyo zao lenye nguvu kwenye soko la Dunia.


Ameongeza kuwa Maafisa Ugani katika kuwawekea mazingira bora ya kutoa elimu kwa mkulima wameongezewa bajeti yao kutoka Shs milioni 600 na sasa ni Shs Bilioni 15 huku wakisambaziwa jumla ya Pikipiki 7,604 zitakazo rahisisha mazingira ya kazi zao.


Akitoa taarifa za Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Balandya Elikana,Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara amesema Mkoa wa Mwanza msimu wa kilimo 2022/2023 unatarajia kulima zaidi ya hekta 67000 za Pamba zenye makisio ya mavuno ya Tani 56,000.


Naibu Waziri Mavunde amegawa zana za kilimo zikiwa ni baadhi kutoka kwenye mradi wa BEYOND COTTON unaofadhiliwa na Serikali ya Brazil zikiwemo mashine za kuandaa shamba 3,zana za kupandia 600, na zana za kupalilia 3 pamoja na Pikipiki 3kwa ajili ya Maafisa Ugani.


Serikali ya Tanzania Julai mwaka huu hadi Disemba 2023 imeingia rasmi mkataba na Nchi ya Brazil wa kuendeleza zao la Pamba pamoja na chakula na lishe,Taifa hilo kutoka Amerika ya Kusini likitoa Dola za Kimarekani 629,000 kugharamia mradi huo ujulikanao kama BEYOND COTTON.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti