• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali yawaahidi fidia sahihi Wakazi wa Satto na Nyabili Wilayani Sengerema kupisha shughuli za Mgodi

Posted on: June 9th, 2022

Serikali imewahakikishia stahiki zao za fidia kulipwa kwa usahihi na mapema Wananchi wa Vijiji vya Sotta na Nyabila vilivyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ambao wanafanyiwa tathmini ya mali zao kupisha shughuli za Mgodi wa Madini.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dktr Angelina Mabula akiongozana na Viongozi  wengine waandamizi wa Serikali amefanya mkutano wa hadhara kuzungumza na Wananchi hao baada ya baadhi yao kushindwa kupata ufahamu sahihi dhidi ya maeneo hayo na zoezi la tathmini kwa ujumla.


Mhe Mabula amesema kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 97 hakuna mtu anayeweza kumiliki maeneo ya Milima,Maziwa,Mito au sehemu za Bahari hivyo ni vyema Wananchi watambue  ili kuepusha migogoro isiyo na tija.

"Nimelazimika kuja kuwapa ufafanuzi huu na kuwaondolea shaka baadhi yenu katika zoezi zima la fidia ambalo kabla Mtathmini Mkuu wa Serikali,Everyn Magasha amelikamisha na hekari moja mtalipwa Shilingi Milioni 2 ikiwa ni nyongeza kutoka Milioni 1.5 ambayo ndiyo bei  ya soko la radhi hii" Mhe Mabula.


Amesema Serikali ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kupigania kuinua Uchumi wa Nchi na Mwananchi imeweka mazingira mazuri kwa Wawekezaji wanaokuja hivyo kazi iliyopo ni kumpa nafasi Mwekezaji huyo aanze kazi mapema iwezekanavyo.


Naibu Waziri wa Madini Dktr Steven Kiruswa amesema tayari Serikali imeshaingia mkataba na Mwekezaji huyo ambaye tayari ametumia Shilingi Bilioni 240 kwa shughuli za Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa yaliyomo ndani ya Mkataba huo.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amesema hii ni fursa nyingine ya kuwainua kiuchumi  Wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo wajibu wao sasa ni kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni Mmbia na Mwekezaji huyo.


Asilimia 85 tayari wameshiriki zoezi la kufanyiwa tathmini ya mali zao kabla ya kulipwa fidia huku asilimia 15 wakiwa bado kutokana na kutopata ufahamu wa kuhusu fidia zao  ambapo sasa wamesha elimishwa na wanatarajiwa kuthaminishwa maeneo yao.

Fidia nyingine watakazo lipwa Wananchi hao ni pamoja na Nyumba,Makaburi,Mazao  stahiki,Posho ya kusafirisha mizigo tani 12, na Posho ya miezi 36 ya kujiandaa na makazi mapya.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti