• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Serikali Yazindua vivuko vya Bugorola- Ukara,Chato- Nkome

Posted on: August 25th, 2019


Serikali  imezindua rasmi ujenzi wa vivuko viwili  vya kisasa  vitakavyofanya safari za kusafirisha abiria , mizigo na magari  kati ya Bugorola-Ukara   Wilaya ya Ukerewe  Mkoa wa Mwanza na Chato-Nkome Wilaya ya Chato mkoani Geita.


Uzinduzi huo umefanyika mkoani Mwanza eneo la karakana ya Kampuni ya Songoro Marine Transport Boaty  Ltd, inayojenga vivuko hivyo ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka Chato  na Ukerewe  walihudhuria hafla hiyo.


Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Mhandisi Japhet Masele alisema Serikali imeamua kujenga vivuko hivyo kutokana na kuwapo na mahitaji makubwa hususani Ukerewe ambapo hivi karibuni kulitokea ajali  eneo la Bugorola na kusababisha vifo  vya watu.


Mhandisi Masele alisema  kivuko cha Bugorola-Ukara   kitajengwa  na Kampuni  ya Songoro Marine Transport Boaty  Ltd kwa Sh. bilioni 4.2 bila kuwapo na Ongezeko la Thamani (VAT) huko kile cha  Chato- Nkome kitagharimu Sh bilioni 3.1.


“Vivuko vyote vitagharimu Sh bilioni 7.3 ambazo zote zitatolewa na Serikali, kwa mujibu wa mikataba tuliyoingia na kampuni hii ni kwamba vivuko hivi vitajengwa kwa miezi 10 tu, hivyo tunamuomba mzabuni wetu  ambaye ni mzawa akamilishe kazi hii kwa wakati.

“Kivuko cha Bugorola-Ukara kitakuwa na na vipimo vya urefu wa mita 39, upana mita 10 na kitaelea ndani ya maji kati ya mita 0-7 hadi 1.0, pia kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abairia 300, magari 10 na mizigo, vile vile kivuko cha Chato-Nkome kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 200, magari 10 na mizigo.


“Vivuko hivi  vitafungwa injini  mbili  na vitaendeshwa na mifumo  miwili ya usukani ambapo moja itakuwa ni ya dharula, kama mtakumbuka nimewaambia tunataka kuimarisha usalama majini na usafiri wa uhakika ndiyo maana vinajengwa kwa mabati maalum ya daraja la kwanza ‘grade  A marine’ hivyo natarajia  Aprili, 2020 tutakabidhiwa,’alisema.


Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Boaty  Ltd,Major Songoro aliipongeza Serikali kwa kumwamini na kumpa zabuni za kujenga vivuko hivyo huku akiahidi kuvikabidhi Februari na si kama mkataba unavyoelekeza Aprili, 2020.


“Kutokana na Serikali kuwa na imani na mimi, naahidi kwamba vivuko hivi navikabidhi Februari, 2020 na si kama mkataba unavyosema nikabidhi Aprili, kama mnavyoona wafanyakazi wameanza kazi rasmi na wana utayari wa kufanya kazi, binafsi naogopa kusema mambo mengi bali nataka vitendo ndio viongee zaidi,”alisema.


Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya amesema  ujenzi wa vivuko hivyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Mhe.Dkt. John Magufuli ya kutaka  kuboresha   na kuimarisha usalama wa abiria na vyombo vya majini ndani ya Ziwa Viktoria.


“Hapa kinachotekelezwa ni ahadi ya Rais wetu na ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatutaki yale yalitokea Bugorola yatokee tena, sote tunajua mahitaji yaliyopo pale Bugorola ingawa kuna kivuko  cha MV. Sabasaba kinafanya kazi pale.


“Kama Serikali  tumekusudia kuwawezesha wakandarasi wa ndani ili fedha hizo ziweze kubaki hapa hapa, pia Mwanza ipo katika mkakati maalumu wa kuwa kituo cha uchumi katika   Nchi za  Afrika Mashariki ndiyo maana tunataka kampuni hii iwezeshwe na kuwa mahiri kwa ajili ya kujenga meli kubwa hapa hapa Mwanza, hivyo tunawaomba viongozi wa kampuni hii wajitahidi sana katika kazi,”alisema.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti