• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Siku ya Ukimwi Duniani,Rai yatolewa Mwanza kuepukana na tabia hatarishi

Posted on: December 1st, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Adam Malima ameiasa jamii kuachana na tabia hatarishi zinazochochea Maambikizi ya VVU/UKIMWI ili kuepukana na athari za janga hilo.

Malima ametoa rai hiyo leo (Disemba 01, 2022) kwenye viwanja vya Mirongo Jijini Mwanza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye viwanja hivyo.

"Kwa takwimu hizi za Maambukizi ya Asilimia 7.2 Mkoani kwetu ambayo ni zaidi ya Asilimia 4 ya Kitaifa inaonesha hali ya Maambukizi kwa Mwanza kuwa bado yapo juu sana hivyo ni lazima tulifanyie kazi suala hili hususani kuwakinga na janga hili watoto wetu ambao ni Taifa la kesho." Malima.

Aidha, ametoa wito kwa wenye Maambukizi ya VVU/UKIMWI kutumia dawa za kufubaza maambukizi ili kuendelea kuzalisha uchumi wao kwa kujitafutia kipato kwa kukuza  mitaji inayosaidia kuboresha maisha yao.

Hata hivyo, ametoa wito kwa mashirika yote Mkoani humo kushirikiana na serikali katika kukidhi matakwa ya kitaalamu na miongozo ya Wizara ya Afya katika kuhudumia Wananchi na amezitaka Halmashauri kupeleka nguvu kwenye afua za kudhibiti maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa ICAP nchini ndugu Michael Kalunga amesema shirika hilo linaendelea kushirikiana na Serikali kupitia kutoa msaada wa vifaa tiba kuhakikisha wanafikia malengo ya kusaidia watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi waweze kufahamu hali zao.

Yasin Ally, Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini amesema Shirika hilo linafanya jitihada katika kuhakikisha wanakemea masuala ya ukatili wa kijinsia kama Ubakaji wenye matukio  479, matukio 1115 ya Mimba za utotoni na 1044 ya Ulawiti mkoani humo ili kuwafanya watoto waweze kustawi.

Akisoma risala ya Maadhimisho hayo, Joseph Kiarata amesema huduma zisizo na vikwazo kwa watoto na jamii kwa ujumla ndiyo lengo la Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kijamii bila ubaguzi.

"Katika 2016 hadi 17 Mkoa wa Mwanza uliongeza maambikizi ya VVU/UKIMWI kwa asilimia 7 lakini Serikali inaendelea kufanya afua mbalimbali za kusaidia kufuta maambukizi mapya kama matumizi ya kondomu, kukemea matumizi ya dawa za kulevya, ndoa za utotoni, ulawiti na Ubakaji na kuhudumia wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti