• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

SUMATRA Yawabana Leseni Feki,Vishoka

Posted on: August 8th, 2018

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu(SUMATRA) imefanya mkutano  kati yao na wamiliki wa magari pamoja na madereva wa  magari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, kwa ajiri ya kutatua changamoto za usafirishaji wa barabarani na kutoa elimu ya maombi ya leseni kwa njia ya mtandao.

Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA  Bw.Gilliad Ngewe amesema kuwa kazi ya SUMATRA ni kusimamia huduma za usafirishaji wa barabara na majini kwa kufuata sheria,kanuni na utaratibu na kutoa elimu ili kuondoa umiliki wa leseni feki na wasio na  leseni na kuwaondoa vishoka.

"Tutadhibiti  mitandao yote feki ya jutoaji leseni,rushwa na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wamiliki wote wa leseni feki, pia kwa kuwafungia vifaa maalum vya kudhibiti mwendo kwenye mabasi ya mikoani, kwa ajili ya kuzuia ajari za barabarani, ili kusaidia kupunguza matumizi  makubwa ya mafuta, matumizi ya matairi mabovu na ufungaji wa breki njiani ovyo,"alisema Ngewe.

Kwa upande wake Meneja wa leseni SUMATRA Leo Ngowi ameeleza jinsi ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kusema kuwa vitu vinavyohitajika kwenye kujaza maombi ya kwa njia ya mtandao ni lazima uwe na Nakala ya kadi ya udereva, Bima ya gari, Nakala ya leseni ya Udereva na Hati ya ukaguzi, kwa kutumia njia hii itasaidia kuondoa leseni feki na kuokoa muda.

Nao wamiliki na madereva wa magari wametoa changamoto zao hasa katika upande wa faini za mara kwa mara za barabarani, kuondoa vishoka, na kuzingatia upande wa walemavu, wawe wanakuja wenyewe SUMATRA barabarani kukagua na kuomba matatizo hayo yarekebishwe na sio kuendelea kuongelewa kila siku bila kufanyiwa marekebisho.

Aidha  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Issa Hamad ameekezea juu ya ukaguzi wa leseni na bima kwa njia ya mtandao.

 "Endapo akiingiza namba ya bima na leseni yako kama ni feki au imeisha muda wake mfumo huwa unasema na matokeo yake unatakiwa kwenda kulipa faini  pia muda mwingine tunakukagua gari lako pasipo kukuambia ila tukigundua kama unakosa huwa tunakulipisha faini na kukupa risiti ukalipie kwa kukwepa malumbano ya kuanza kukuelezea kosa tutachukua mda mrefu,"alisema Hamad.

Mkuu  wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza  ACP M.K. Mkadam amesema anahitaji wampelekee magari ya polisi yanayofanya makosa, anahitaji watendaji wake wafanye kazi na ametoa namba ya simu kwa wananchi kwa ajiri ya kuwashitaki madereva ambao hawafikishi katika vituo wanavyohitaji kushuka, na alisisitiza kutoa elimu zaidi ili waende na wakati.

Hata hivyo Mhe.Ngewe amemalizia kwa kuwataka madereva na wamiliki wa magari wafuate sheria, kanuni na utii ili kuondoa matatizo ya barabarani na waache kutoa rushwa hivyo itasaidia kuondoa leseni feki na vishoka.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti