• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TAKUKURU Yafanikiwa kurejesha zaidi ya milioni 17 za mstaafu alizozulumiwa

Posted on: April 8th, 2020

Zaidi ya million 17 alizotapeliwa Mwalimu mstaafu zarejeshwa na Taasisi ya kuzuia na  kupambana na rushwa (TAKUKURU) yamrejeshea.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Emmanuel Stenga alisema walipokea taarifa  kutoka kwa msiri kuwa mwalimu mstaafu Masolwa Lukanda (62) amedhulumiwa mafao yake na mtu aitwaye Bosco Marwa (32)ambapo jumla ya million 32 zilichukuliwa kwenye akaunti yake kwa njia isiyo halali .

Alisema uchunguzi uliofanywa na taasisi hiyo ilibaini kuwa mzee huyo alikuwa ni mtumishi wa shule ya msingi Bulolambeshi iliyopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo alistaafu kwa lazima Julai 19 mwaka juzi na kulipwa mafao yake na Mfuko wahifadhi ya jamii PSPF  Febuary 22 mwaka jana ,Mwl huyo alikuwa na mikopo halali kwenye taasisi za fedha na mikopo hiyo ilikatwa kwenye malipo yake ya kustaafu na kubaki na 40,603,821,92.

Aidha alisema mbali na mikopo ya taasisi za fedha aliingia mkataba wa mkopo baina yake na Mmiliki wa Zabo Microcredit Ltd Bosco Marwa na alikopeshwa 14,559,625 ambapo mkatapa huo wa Agosti 27 mwaka juzi haukuonyesha riba bali una masharti kuwa fedha za mikopo zitarejeshwa baada ya mkopaji kupata malipo ya kustaafu.

“Machi 12 mwaka jana mwl huyo alipokea hundi ya mafao yake ya kustaafu ofisi za  Tume ya Utumishi  wa Walimu wilayani humo alipotoka nje ya ofisi alimkuta Bosco Marwa anamsubiri na akamtaka waende moja kwa moja benki akamlipe fedha zake ambapo siku hiyo kulikuwa na tatizo la kiufunza hawakuwaza kutoa fedha hiyo ambapo kesho yake waliongozana hadi tawi la NMB Kenyatta jijini Mwanza ambapo Bosko alichukua Tsh 32,000,000 kurejesha deni la Tsh.14,5559,625 hivyo kupokea malipo yasiyo halali ya Tsh 17,440,375.”alisema Stenga.

Aliongeza kuwa baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na kubaini ukweli wamalalamiko hayo mtuhumiwa alikiri kuchukua fedha hizo na kuagizwa azirejeshe mara moja tayari fedha hizo zimerejeshwa na kukabishiwa mwl huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefurahiya na kuipongeza TAKIKURU kwa kazi wanayofanya katika Mkoa huo.

"Kwanza niwapongeze sana TAKUKURU kwa kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kufanya kwenye Mkoa wetu,mmeona kwenye matukio mengi tu wamesaidia sana kupata mali za umma ambazo wakati mwingine zimechukuliwa kinyemela,mnakumbuka tukiwa katika zoezi la vyama vikuu vya ushirika mpala leo hapa,mnakumbika madeni ya wakulima kwenye sekta ya pamba TAKUKURU imefanya kazi kubwa sana Mkoani,"alisema Mongella.

"Leo tumeona tena fedha takribani milioni kumi na saba laki nne elfu arobaini mia tatu sabini na tano(17,440,375) Sh. za Kitanzania ambazo Mzee Masolwa Ngeleja Lukanda alitapeliwa au aliibiwa na Bwana Bosco Michael Marwa ambaye ana Kampuni ya Zabo Microcredit LTD. Huu ulikuwa ni wizi tu wa mchana," alisisitiza.

"Mimi nitoe rai hapa kuna dalili hata kwenye mifumo yetu wenyewe kina mazingira ya ovyo kwa sababu huyu mzee katika mazingira ya kawaida alitakiwa kuambiwa na mwajiri wake pale Halmashauri au mfuko wa PSPFkwamba fedha yako imetoka maana wale ndiyo walitakiwa kumlipa lakini inaonekana huyu bwana alikuwa na mlolongo wa kujua kule na alikuwa ameishapanga kumchukulia fedha huyu mzee sasa TAKUKURU wakapa taarifa kwa mtoa taarifa,msiri na tunamshukuru sana,"alisema Mongella.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti