• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Tanzania Yataka mataifa yanayoshiriki maonesho,TCCIA Kujenga viwanda

Posted on: September 18th, 2019


 Serikali imezitaka kampuni kutoka mataifa ya Kenya, Uganda,  China, Egypt na India ambazo zimekuwa zikishiriki maonesho ya Afrika Mashariki yanayoandaliwa na  Chemba ya Wafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na yale ya kimataifa ya  Biashara ya Dar es Salaam (DITF) maarufu Sabasaba kujenga viwanda vyao nchini.

Kauli  hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade),  Edwin Rutageruka ambaye alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa katika ufunguzi wa maonyesho ya 14 ya TCCIA yanayofanyika katika viwanja vya jengo la biashara la kimataifa la Rocky City Mall, jijini Mwanza.

Rutageruka amesema  sababu ya Serikali kuzitaka kampuni hizo  kujenga viwanda vyao nchini  kutokana na  bidhaa zao zinakubalika kwa watanzania na zaidi katika kushindanisha washiriki wa maonyesho mbalimbali  zimekuwa zikiibuka na ushindi wa jumla  na kujizolea  vikombe   vingi.

Alisema  hakuna haja ya kampuni hizo kuendelea kupata usumbufu wa kusafirisha bidhaa zao kila mwaka kuleta Tanzania kwa ajili ya maonyesho, hivyo ni wakati muafaka wa kuwekeza nchini kwa kujenga viwanda ikiwa ni sehemu ya uwekezaji kwani tayari soko limepetikana.

“Ninachozungumza hapa ni  cha waziri Bashungwa ambaye anasema wakati Serikali inawakaribisha wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kuja kuwekeza nchini kutokana na bidhaa zao kukubalika, ni wakati muafaka kwa watanzania kujifunza na kuiga kile kinachofanywa na wenzetu, tusiendelee kupenda vya wengine na kusahabu vya kwetu.

“Mimi ni mzoefu katika maonyesho haya ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, ukifika katika mabanda ya washiriki wakigeni unakuta watanzania wamefurika pale wakinunua bidhaa zao, mfano kampuni ya Movit ya Uganda inakuwa na wateja wengi, sasa hakuna haja kila mwaka kusafirisha bidhaa, kama Serikali tunawataka waje tuwape maeneo ya kujenga viwanda vyao.

“Tanzania ni salama na inawakaribisha wawekezaji kutoka Kenya, Uganda,  China, Egypt na India kwani hawa kila mwaka wanapata vikombe vya washiriki na bidhaa bora, hata leo sote tumeshuhudia hapa zawadi nyingi zimechukuliwa na kampuni za nje, naomba viwanda vijengwe hapa Mwanza kwani ndio kitovu cha nchi za Afrika Mashariki,”alisema.


Katika hatua nyingine, Rutageruka alisema sekta ya kilimo inaendelea  kukosa mvuto kwa watanzania na  wengi wao wamegeukia biashara ambapo aliwashauri viongozi TCCIA wanaoshughulikia sekta ya kilimo kuendelea kuhamasisha wananchi  kuachana na kilimo cha jembe la mkono na kulima kisasa.


Wakati huo huo,alisema asilimia 70 ya wafanyabiashara wa mipakani ni wanawake ambao wengi wao wanafanya shughuli za kiuchumi zisizo rasmi hivyo aliwataka viongozi wa TCCIA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwalimisha  ili kutambulika.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari alisema changamoto iliyopo kubwa  ni washiriki kutoka nje ya Tanzania kusumbuliwa mipakani wanapotaka kuingiza bidhaa  zao kwa ajili ya maonyesho  hayo  kwani huchukua muda mwingi kuthibitisha bidhaa.


Dkt. Mmari aliendelea kuiomba  Serikali kuwapatia  eneo la Nyamhongolo jijini Mwanza ambalo limekuwa likitumika katika maonyesho ya  wakulima maarufu nane nane ili kuliwekeza  katika hadhi ya kimataifa.


Dkt. Mmari alisema miongoni mwa fursa zitakazopatikana kutokana na maonyesho hayo ni kuimarisha mtandao wa masoko na usambazaji bidhaa,  kampuni za Tanzania kujifunza na kutanua wigo wa biashara kwa kutumia  makubaliano ya kibiashara ya kimataifa.


Vile vile alisema kufanyika maonyesho hayo yanatoa mchango kwa vitendo katika kuunga mkono juhudi za Rais Mhe. Dkt. John Magufuli kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati ifikipo 2025 sambamba na kuimarisha mtengamano wa soko la pamoja la Afrika Mashariki.





Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti