• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TARURA KILIMANJARO WAJIFUNZA UJENZI WA BARABARA ZA MAWE MWANZA

Posted on: September 6th, 2023

TARURA KILIMANJARO WAJIFUNZA UJENZI WA BARABARA ZA MAWE MWANZA


Leo Septemba 06, 2023 wafanyakazi 25 kutoka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Kilimanjaro wamewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya siku 1 ya mafunzo ya namna ya kujenga barabara kwa kutumia teknolojia ya mawe hususani kwenye maeneo ya miinuko.

Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Miundombinu, Mbunifu Majengo Chagu Nghoma amesema Teknolojia hiyo inasaidia kuwafikia wananchi wanaoishi kwenye miinuko kutokana na kuwapelekea barabara ya kudumu kwa gharama nafuu tofauti na siku za nyuma ambapo walijengewa kwa udongo na changarawe na kupelekea kutodumu kwa muda mrefu.

Vilevile, amebainisha kuwa kutokana na kufikika kwenye maeneo hayo kutokana na uwepo wa barabara, inaweka pia mazingira rahisi ya kupeleka huduma za jamii kama Shule, Masoko, Maji na Umeme kwenye makazi ya miinuko kutokana na mipango miji kuwa inayoeleweka tofauti na kwenye makazi ambayo kunakua na barabara za asili zisizopitika kwa urahisi.

"Ujenzi wa barabara hizi unasaidia sana kutumia nguvu kazi za wananchi kwenye eneo husika kwa ajira za muda na inailetea sifa Serikali kwa kutekeleza miradi hiyo kwa kundi kubwa la wananchi wanaoishi kwenye makazi ya miinuko ambao hali zao wengi ni za chini kiuchumi." Amefafanua Nghoma.

Meneja wa TARURA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Goodluck Mbaga amesema Teknolojia ya Ujenzi wa barabara za mawe ni nzuri na nafuu kwani kwa barabara ya Kilomita Moja inagharimu wastani wa Milioni 360 tofauti na gharama za kujenga barabara za kiwango cha Lami ambayo hugharimu zaidi ya Milioni 800 kwa Kilomita.

"Teknolojia hii ni nafuu na bora sana yaani inakupa uwezo hata wa kuyatumia mawe hayo kwa shughuli zingine baada ya muda wa barabara kuisha na tunawashukuru sana wetaalamu walioileta teknolojia hii hapa nchini miaka ya 2007 ambapo ilijengwa barabara ya kwanza Kigoma kabla ya mwaka 2008 kuitumia mkoani Mwanza." Mhandisi Mbaga.

Meneja TARURA Kilimanjaro Mhandisi Francis Nicholas amesema ziara yao ina tija kwani wamekuja Mwanza kujifunza namna ya kutumia teknolojia ya ujenzi wa barabara za mawe huku akibainisha kuwa wana maeneo ya miinuko na wana utajiri wa mawe mkoani kwao hivyo wameona waje wajifunze namna ya kutekeleza hususani kuyadhibiti maji.

Amesema kuwa Same na Mwanga ni miongoni mwa wilaya zenye jiografia ya milima na mawe mengi na katika kutimiza adhma ya kumsaidia Mhe. Rais Samia kutekeleza miradi ya barabara kwa gharama za chini lakini kwenye ubora hivyo wameona waangazie kwenye matumizi ya teknolojia hiyo ambayo huzalisha barabara za kudumu muda mrefu.

Awali Mhandisi David Christopher kutokka Ofisi ya Meneja wa TARURA Mwanza alielezea kuwa Mkoa huo una barabara zenye Urefu wa Kilomita 18.74 na kwamba halmashauri ya Jiji la Mwanza ilikua ya kwanza kujenga barabara zenye Urefu wa Kilomita 1.5 Mwaka 2008 kabla ya kuanzishwa kwa TARURA.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti