• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TCRA Yawaonya matapeli wa Mitandao

Posted on: June 13th, 2019

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuanzia Januari Mosi, 2020  kila mtu atatakiwa kumiliki laini moja ya kampuni moja ya simu ya mkononi.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TCRA kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo katika mkutano  wa wadau wa sekta ya mawasiliano  uliolenga kupokea kero na mapendekezo juu ya utendaji wa mamlaka hiyo.

Mkutano huo ulishirikisha viongozi wa dini mbalimbali,wamiliki wa vituo vya redio, mitandao ya kijami na mafundi simu ambapo wengi wao waliomba TCRA kushirikiana na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuweza kupata vitambulisho kwa wakati.

Mhandisi Mihayo alisema kwa mtu atakaye hitaji kuwa  na laini mbili atatakiwa kuandika maelezo ya uhitaji huo.

Alisema, imelazimika kuunda kundi maalum ‘group’ linaloshirikisha watoa huduma za mawasiliano  nchini kwa ajili ya kuziharibu simu za matapeli  wanaotuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwa watu ili kujipatia fedha  kwa njia zisizo rasmi.

Pia imewaonya watu maarufu  wakiwamo wanasiasa wanatumia mitandao ya kijamii  kusambaza taarifa ambazo zinapotosha jamii kuhusu jambo lolote na kuwataka kuacha mamlaka husika au vyombo vya habari kusema kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.

“Moja ya malalamiko sugu katika suala la mawasiliano ni watu kutumia ujumbe wa utepeli, kweli watu wametapeliwa sana, wapo wanaolalamika kupata ujumbe usiku na kusababisha  mgogoro katika ndoa lakini kama TCRA na watoa huduma tukaamua kuunda group letu la kuwashughulikia watu wa namna hiyo”alisema

Mhandisi Mihayo alisema TCRA  imeendelea kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano, kuchapisha majarida, vyombo vya habari lengo likiwa ni kujua namna ya kutumia sekta ya mawasiliano kwa faida na kuziomba taasisi za dini  kuelimisha waumini wao.

Alisema  mmomonyoko wa maadili  katika familia umetokana na wazazi kuwaruhusu  watoto wadogo kutumia simu za mikononi jambo ambalo linawafanya kuangalia picha za ajabu.

Mhandisi Mihayo alisema, baadhi ya watu maarufu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuandika mambo yasiyo ya kweli  huku jamii  ikiwaamini kuliko vyombo vya habari vyenye leseni na kuwataka kuwa makini na taarifa wanazoweka mitandaoni kwani wanawafuatilia kwa ukaribu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti