• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TIMIZENI NDOTO ZA RAIS SAMIA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI : KATIBU MKUU TAMISEMI

Posted on: April 5th, 2024

TIMIZENI NDOTO ZA RAIS SAMIA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI : KATIBU MKUU TAMISEMI


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Aprili 5,2024  amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Kanda ya ziwa (LVRLAC) na kutoa rai kwa wajumbe kuhakikisha wanatimiza ndoto za Rais Samia za kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na miradi iliyoelekezwa kwenye Halmashauri zao.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu (OR-TAMISEMI) Balandya amesema Serikali ya awamu ya sita imeleta miradi mingi hasa mkoa wa Mwanza hivyo ni wajibu kwa wakurugenzi, Meya na Madiwani kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa kikamilifu ili iwe na tija kwa wananchi.

"Ndugu wajumbe wa LAVRLAC Tanzania tuna bahati ya  ziwa Victoria sehemu kubwa kuwa huku kwetu,fursa za uchumi wa bluu umezidi kuongezewa nguvu kwa Serikali kuiboresha sekta ya uvuvi kwa ufugaji wa samaki kutumia vizimba,juhudi hizi ni lazima zilete matokeo chanya kwa usimamizi mzuri kwetu sisi tuliopewa dhamana ya uongozi",amesisitiza mtendaji huyo wa mkoa.

Balandya ameipongeza Jumuiya hiyo kwa juhudi zake za kuziwezesha Halmashauri miradi iliyofikia thamani ya zaidi ya shs bilioni 20 huku ikiendelea na mikakati ya utunzaji mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

"Hizi safari zenu za mara kwa mara nje ya Tanzania niwasihi mzitumie vizuri kujifunza kutoka kwa webzetu waliopiga hatimua katika utaalamu hasa mabadiliko ya tabia nchi,wananchi wetu wanajikuta wanaharibikiwa na mazao au kutokea kwa ukame,"amesisitiza Balandya.

Mtendaji Mkuu wa LAVRLAC Bill Brown amesema mkutano huo mkuu wajumbe watapata nafasi ya kujadiliana changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kumletea maendeleo mwananchi.

"Wizara hii ya Tamisemi inatengewa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo,hivyo nyie Wakurugenzi na Madiwani tunawahimiza mkasimamie kwa umakini na uadilifu mipango hii ya kuwaletea maendeleo wananchi,"Steven Matambi,Kaimu mkurugenzi wa Serikali za mitaa,Tamisemi.

Washiriki wa mkutano huo  ni wakurugenzi wa Halmashauri,Madiwani,Wenyeviti wa Halmashauri wanatokea mikoa ya Mwanza,Kagera,Simiyu,Mara,Geita na Shinyanga.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti