• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TUTUMIE MATAMASHA KUUTANGAZA UTAMADUNI WETU - DKT. BITEKO

Posted on: June 27th, 2024

TUTUMIE MATAMASHA KUUTANGAZA UTAMADUNI WETU - DKT. BITEKO


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko ametoa rai kwa Watanzania kutumia  matamasha makubwa kama la Bulabo (Tamasha la sherehe za mavuno) kutangaza mila na tamaduni za Mtanzania, ikiwa ni njia muhimu ya utambulisho wa Taifa la Tanzania kimataifa.

Mhe. Biteko ametoa rai hiyo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania (Chifu Hangaya) katika kilele cha Tamasha la Utamaduni la Bulabo Kanda ya Ziwa lililofanyika leo Juni 27, 2024 Bujora - Kisesa Wilayani Magu Mkoani Mwanza.

Mhe.Biteko amesema Taifa la Tanzania lina mila na tamaduni zake ambazo hurithishwa vizazi kwa vizazi ambapo ni lazima zilindwe na zihifadhiwe vizuri na kujiepusha na kupokea tamaduni za kigeni ambazo sio asili yetu.

"Ni lazima tulinde na kudumisha tamaduni zetu, Taifa lisilodumisha tamaduni zake, hilo ni Taifa la mazombi, hivyo ninawaasa tudumishe misingi ya mila, desturi na tamaduni zetu". Amesema Mhe. Dkt. Biteko.

Aidha Dkt. Biteko ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa Mkoa Mtanda kwa maandalizi mazuri na ya kiwango ya tamasha hilo la bulabo na kuahidi kwenda kuyasimulia hayo kwa Mh. Rais Samia, sambamba na hayo pia ametoa maagizo kwa Mikoa yote ya kanda ya ziwa kuhakikisha wanashirikiana vizuri katika kuandaa tamasha hilo kwa mwaka ujao ili kulifanya  kuwa la viwango.

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema wamedhamiria kulikuza na kuliendeleza tamasha hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo na kulitangaza pia kimataifa ili nalo lifanywe kuwa ni kivutuo cha utalii kwa kanda ya ziwa.

"Nina hakika mwakani tamasha hili litakua bora zaidi na niwahakikishieni kuwa tutatarajia kupokea zaidi ya watalii 100 kutoka nchini Brazili watakaokuja kushiriki katika tamasha la bulabo, lengo ni kuutangaza utamaduni wa kabila la kisukuma kimataifa".

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti