• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Uhifadhi wa Misitu wahimizwa Mwanza

Posted on: January 30th, 2022

Naibu Waziri wa Maliasili na Utaliii Mhe. Mary Masanja ametoa rai kwa viongozi wa Kanda ya Ziwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto za uhifadhi wa mazingira hususan katika mkoa wa Mwanza na Simiyu, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya kila kiumbe ya sasa na siku za usoni.

Rai hiyo imetolewa leo mara baada ya kupokea taarifa ya Hali ya Uhifadhi  mkoani Mwanza ambapo Waziri alizitaka jamii za wakulima na wafugaji zinazoishi maeneo ya Hifadhi za Misitu ziishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Mhe. Masanja anasema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wananchi wa vijiji vinavyouzunguka msitu nchini ni elimu juu ya uhifadhi na athari zake, namna wanavyoweza kutumia hifadhi za misitu kutokomeza umaskini pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya ardhi.

Kufuatia hali hiyo, Waziri ametoa rai kwa uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS, viongozi wa Wilaya na Vijiji kushirikiana pamoja kuelimisha wananchi wanaozungumza hifadhi za misitu huku Wakala ukitakiwa kutafuta miradi kupitia programu za kurudisha kwa jamii (CSR) kusaidia jamii kando mwa misitu.

“Ninafahamu kuwa kuna Kamati ya Mawaziri nane iliyoundwa kushughulikia migogoro ya mipaka katika hifadhi yza misitu, lakini wakati tukishubiri kamati hiyo kutoa mapendekezo yake, tuanze sasa kutoa elimu na kuwafanyia vitu vingi vya CSR ikiwemo kuwapelekea miradi ya Ufugaji Nyuki pamoja na Kilimo na Ufugaji bora ili watuelewe, na wajue tunapohimiza uhifadhi tuna lengo zuri,” anasema Mhe. Masanja.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel anasema misitu iliyopo Kanda ya Ziwa haina hali nzuri na kuwataka viongozi kuchukua hatua za kuhimiza uhifadhi.


“Msitu yetu tumeiona kwenye ramani kubwa ya Kanda ya Ziwa hapa, niwaombe viongozi tuwe na moyo wa kihifadhi, kanda hii kuna maeneo yalikuwa na mvua mara mbili kwa mwaka na sasa mvua ni zakubahatisha huku maeneo mengine yakikumbwa na ukame, hakuna muujiza ni uhifadhi. Kuna maeneo yalikuwa na mito mikubwa sasa imekauka na ng’ombe wamekufa, tuna haja kubwa yakuwekeza kwenye mabadiriko ya tabia nchi,” anasema Mhe.  Mkuu wa Mkoa.

Anaongeza kwa kusema kuwa “viongozi wote kwa pamoja tuwe na wimbo mmoja, waheshimiwa wabunge, viongozi wa Serikali Kuu, taasisi za umma na binafsi tushirikiane sote kwa pamoja tuhifadhi misitu yetu kwa faida ya kizazi kijacho ambacho tusipofanya maamuzi magumu leo hii hakitakuwa na furaha, tusiwe wabinafsi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.  Salum Kali, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria na wabunge wawakilishi wa wananchi wanaoishi kando mwa hifadhi za misitu walisema, uhifadhi nchini una faida kubwa, muhimu ni kuwepo na programu ya kutoa mafuzo ya uhifadhi sambamba na kuanzisha miradi yenye manufaa katika uhifadhi wa misitu na kuleta manufaa kwa wananchi.



Awali Kamishna wa Uhifadhi – TFS Prof. Dos Santos Silayo alisema Wakala uko tayari kushirikiana na viongozi wa Kanda ya Ziwa katika kuhakikisha kuhakikisha uhifadhi unafanikiwa.

Aidha alisisitiza  kuwa licha ya changamoto mbalimbali za uhifadhi nchini, Wakala utaendelea kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu na nyuki ili kuchangia kikamilifu mahitaji ya kijamii, kiuchumi, kiikolojia na kiutamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti