• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Utapiamlo bado ni changamoto kwenye vituo vya kulea watoto nchini: Katibu Mkuu SMZ

Posted on: February 29th, 2024

Utapiamlo bado ni changamoto kwenye vituo vya kulea watoto nchini: Katibu Mkuu SMZ


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  Abeida  Abdallah amesema bado inahitajika nguvu ya wadau wa maendeleo kukabiliana na changamoto ya utapiamlo kwa watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali nchini.

Akizungumza na wafanyajazi kwenye kituo cha Anza kwa Imani kilichopo wilayani Misungwi Mtendaji huyo mwandamizi wa Wizara amesema utapiamlo bado ni tatizo  hivyo amewaomba wadau na wananchi wenye uwezo kusaidia upatikanaji wa mahitaji kwa watoto ikiwemo chakula, mavazi na matibabu.

"Natoa wito Serikali tunahudumia, lakini pia wananchi ambao wanauwezo wajitokeze kusaidia vituo  ili watoto wapate lishe bora" amesema Bi. Abeida.

Katika ziara yake fupi Mkoani Mwanza Katibu Mkuu huyo ametembelea makao ya wazee wasiojiweza yaliyoko Bukumbi wilayani Misungwi  na kutoa Rai kwa wazee hao kuendelea kutunzwa ili waepukane na magonjwa nyemelezi huku akisisitiza ulaji wa mlo kamili pamoja na matumizi ya mboga za majani kwa wingi ili kulinda afya zao  ambao ni tunu kubwa katika Taifa.

Aidha, Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Daniel Machunda akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo amempongeza Katibu Mkuu huyo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (smz) kwa kuuchagua Mkoa wa Mwanza kuja kutembelea makao mbalimbali ya watoto pamoja na makao ya wazee Bukumbi ambapo amesema Serikali ya mkoani humo  inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha vituo vya watoto pamoja na makao ya wazee Bukumbi wanapata mahitaji stahiki ikiwemo mavazi na chakula.

Naye Grace Chenya ambaye ni Afisa Ustawi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalumu amebainisha Serikali inaendelea kusimamia na kuhakikisha watoto wanapata malezi bora ikiwemo huduma za afya na elimu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti