• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Uunganishwaji wa Meli mpya ya MV.Mwanza Hapa Kazi Tu waanza

Posted on: September 16th, 2020


Ujenzi rasmi wa meli kubwa kabisa katika ziwa Victoria waanza rasmi Baada ya kukamilika kwa uwekaji wa mkuku ( Keel Laying ) wa meli mpya ya "Mv.Mwanza hapa kazi tu "inayojengwa katika chelezo.

Akizungumza katika hafla hiyo leo  Ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya huduma za meli ( MSCL) Eric Hamissi anaeleza kuwa hiyo ndio hatua ya kuanza kwa ujenzi na uunganishaji wa msingi wa meli ili kupata msingi wote wa meli ,ambapo kwenye msingi huo utakuwa na kwenye vipande na una  kina cha mita 3.75 ambacho ufikiwa wakati meli imebeba mzigo wote.

" Kukamilika kwa msingi huu wa meli kutawezesha ujenzi wa meli kwenda kwa kasi kuliko kasi ya awali ,kutokana nausanifu bora wa meli hii kampuni yetu inampango wa kuweka kumbukumbu za mradi mzima wa ujenzi wake katika maktaba zake kwa ajili ya vizazi vijavyo " anaeleza Hamissi

Ameongeza kuwa kampuni inayofanya kazi ya ujenzi wa meli hiyo inaitwa GAS Entec, na kampuni ya KANGNAM Corporation zote kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na SUMA JKT ya Tanzania kwa gharama ya Dola za kimarekani 39,000,000 sawa na shilling Billion  89.764 hadi sasa mradi umefikia kiasi cha asilimia 68 kwa ujumla wake na serikali imeshamlipa mkandarasi jumla ya shilingi za kitanzania billion 59.896 sawa na asilimia 68 ya gharama zote za mradi.

Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Dk Leonard Chamiriho anasema hiyo ni hatua ya kwanza muhimu kwa maisha ya meli ,pia mpaka Sasa miradi mitatu imekamilika ambayo ni mradi wa Mv.Victoria ambayo kwa sasa inafanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Bukoba, ukarabati wa mkubwa wa Mv.Butiama na mradi wa chelezo.

" Mji wa Mwanza umenufaika na ujenzi wa meli hii kwani imetoa ajira kwa wingi lakini hapa tulipo Septemba 3 mwaka 2018 ilitiwa saini mikataba ya miradi minne ambapo miradi mitatu imekamilika " ameeleza Chamiriho.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewahakikishia usalama katika mkoa wake ili kazi zifanyike kwa utulivu na ueledi unaotakiwa ,pia ujenzi huo wa miundombinu ya kimkakati ya kiuchumi ni hatua moja wapo nyeti ya kufikia lengo.

" Juzi Rais Magufuli alipofika Mwanza kufanya Kampeni aliwaeleza wananchi nia yake ya dhati na ya serikali kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi kwenye Kanda za maziwa makuu na lengo hilo litatimia" anaeleza Mongella.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti