• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Uzinduzi wa Maadhimisho ya Nanenane Mwanza wafana

Posted on: August 4th, 2022


Mkuu wa Mkoani wa Mwanza Mheshimiwa Adam Malima, amewataka wakulima kuendelea kufuata kanuni bora za kilimo wanapolima mazao ya chakula na biashara ili kuongeza tija ya uzalishaji.

Akizungumza leo Agosti 4, 2022  wakati akifungua  maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima nane nane kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika Viwanja vya Nyamhongolo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Mheshimiwa Malima amesema Sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ndizo zinazoajiri nguvu kazi kubwa hapa nchini  kuliko sekta zingine ambapo kati ya asilimia 63 hadi 65 imeajiriwa na hutegemea kupata riziki katika Sekta ya Kilimo.


"Hivyo uwekezaji katika Sekta ya Kilimo itasaidia sana kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza pato la taifa na kupunguza umaskini katika Kanda ya Ziwa Magharibi inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera pamoja  na taifa kwa ujumla ambalo ndilo lengo la Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshiwa Samia  Suluhu Hassan," amesema Mhe.Malima.

" Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili nchi yetu iendelee kukua kiuchumi kufikia maendeleo ya viwanda ambapo malighafi za viwanda hivi viweze kutokana na sekta ya kilimo ikiweo uvuvi na mifugo,"amefafanua Mheshimiwa Malima.

Mheshimiwa Malima amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya nane nane mwaka  huu isemayo 'Ajenda 10/30: Kilimo ni biashara ,Shiriki kuhesabiwa kwa Mipamgo Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 'inawajulisha wananchi na wakulima kwamba Serikali inalenga kuona Sekta ya Kilimo inakuwa kwa asilimia 10 kufikia mwaka 2030.

"Fursa zilizopo Kanda ya Ziwa Magharibi zinazoweza kuchangia katika ukuaji wa Sekta ya Kilimo ni pamoja na uwepo wa Ziwa Victoria linaloweza kutumika katika kilimo cha umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa  ukame pamoja na ufugaji wa samaki hasa kwa njia ya vizimba.

" Fursa nyingine katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu hasa Ajenda 10/30 Kilimo ni biashara ni kwamba Kanda ya Ziwa Magharibi ni Kituo katika nchi za Maziwa Makuu, Afrika Mashariki, Mikoa na Kanda za jirani na katika nchi za Maziwa Makuu  pamoja na  Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo ni rahisi kuuza mazao ya sekta ya kilimo katika nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda," Mhe. Malima amewaambia Wakulima.

Aidha amewataka wakulima kunufaika na uwepo wa Taasisi za fedha zaidi ya 24 zinazofanya kazi katika Kanda hiyo kwa kukopa mitaji itakayowawezesha kuwekeza katika sekta ya kilimo huku akiwasisitiza wananchi wote kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufayika Agosti 23, 2022  ili Serikali ipate takwimu zitakazoiwezesha kupanga Mipamgo ya Maendeleo.


Vilevile amewataka wananchi wa Kanda ya Ziwa Magharibi kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 kwa kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo ili wafanye shughuli za kiuchumi bila kikwazo.


Awali akitoa taarifa ya maonesho hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nane Nane 2022, Kanda ya Ziwa Magharibi, Emil Kasagara, amesema maonesho hayo ambayo yalianza rasmi kwa kanda hiyo mwaka 2017 yamekuwa yakikumbwa na chamgamoto mbalimbali hususani ukosefu wa Miundombinu  ya kudumu hali hiyo huongeza gharama za uratibu hasa wakati wa ujenzi au ukarabati wa miundombinu Mara kwa Mara.


Akizungumzia mafanikio ya Maonesho hayo,2022, Kasagara amesema hadi Agosti 3,2022 idadi ya washiriki walikuwa zaidi ya 228 ikijumuisha Mamlaka za Serikali za Mitaa wenye shughuli  kubwa na za kati, Taasisi za fedha elimu,afya, kampuni za zana za kilimo,usambazaji pembejeo vinywaji na kampuni za mawasiliano.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwa nza Bwana Balandya Elikana amemshukuru Mhe.Rais  kwa kumchagua kuja kuendeleza maendeleo ya Mkoa wa Mwanza na kuwaomba wananchi kuonyesha ushirikiano katika kuleta maendeleo ya Mkoa wa Mwanza.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti