• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Vijana Ilemela wanufaika na mradiwa Mkwanja

Posted on: May 13th, 2021


Katika kuhakikisha vijana wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na tatizo la ajira jumla ya vijana 181 wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wamenufaika na mradi wa vijana na mkwanja.


Mradi huo wa miaka mitatu ulioanza 2019 hadi 2021,unaotekelezwa na shirika la Mtandao wa Vijana na Watoto Mwanza (MYCN) kwa ufadhili wa The Foundation for Civili Society ambao umegharimu jumla ya milioni 79.


Akizungumzia jijini Mwanza Ofisa Miradi wa MYCN Generosa Ladislaus, amesema mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambapo inahusisha jumla ya kata sita(6) ikiwemo Buswelu,Nyasaka, Ilemela,Shibula,Kitangiri na Nyamanoro.


Generosa amesema,lengo kuu la mradi huo ni kuwakwamua vijana kiuchumi  ndani ya manispaa hiyo hususani kwa kuhakikisha vijana wajasiriamali wanapata fursa za masoko,kujikwamua kimaisha,kumiliki mali na rasilimali.


" Vijana 181 wameweza kufikiwa  moja kwa moja katika kipindi cha mwaka wa utekelezaji ikiwa vijana wa kike 93 na wakiume 88,huku jumla ya vijana 1420 wamefikiwa kwa njia ya mitandao ya kijamii,redio na vipindi vya televisheni  hivyo kufanya jumla ya vijana 1,601 kufikiwa," amesema Generosa.


Pia amesema,vijana wameweza kuanzisha biashara mbalimbali ikiwemo utengenezaji na uuzaji wa unga lishe,siaga ya Karanga,mvinyo wa zabibu na rozela,viungo vya chakula na chai,unga wa soya,majani ya chai,mafuta ya kujipaka mwilini na kwenye nywele,vikapu na viti ,sabuni za maji ,batiki,ufugaji wa kuku,uuzaji wa kuku na nafaka pamoja na uuzaji wa urembo na nguo.


Aidha amesema, miongoni mwa changamoto zilizojitokeza  wakati wa kutekeleza mradi huo ni pamoja na taratibu za upatikanaji wa vibali vya uthibiti ubora,mashine za uzalishaji na vifungashio pamoja na mlipuko  wa virusi vya Corona(COVID-19) ambao umechangia kikwamisha ufikiwaji na uhusishwaji wa idadi kubwa ya vijana.


Mkurugenzi Mtendaji wa MYCN Brightius Titus, amesema mradi huo umegharimu milioni 79 ambapo umetekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza uligharimu milioni 40 ulitekelezwa kwa miezi 6 Julai hadi Desemba 2019 huku awamu ya  pili  ambayo ilitumia milioni 39 ilianza Julai 2020 hadi Machi 2021.

Titus amesema,waliamua kuja na mradi huo baada ya  uwepo wa vijana kushindwa kuendelea na masomo pamoja na wimbi la ukosefu wa ajira,kwanza walihakikisha vijana wanapata elimu ya utambuzi,kuwafundisha namna gani watatumia rasilimali za ndani kulingana na maeneo yaliyopo kisha wakawapeleka SIDO kupata mafunzo ya uzalishaji na masoko huku Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ikawapa mitaji  vikundi vitano kati ya sita kupitia mikopo ya asilimia 4 ya vijana inayotolewa na Halmashauri ili kufanya shughuli za uzalishaji.


"Kilicho tusukuma sisi kuja na mradi wa vijana na mkwanja ni ukitizama takwimu zinaonesha vijana wengi nchini Tanzania wanakabiliwa na wimbi la ukosefu wa ajira kwaio wanaishi katika wimbi kubwa la umasikini,wakaona moja ya kipaumbele cha vijana kujikwamua ni kuwawezesha kiuchumi na tunategemea kuingia awamu ya tatu ya mradi huu ambao utaenda kwa muda wa miaka mitano,"amesema Titus.


Pia amesema,matokeo chanya ambayo yamepatikana ni vijana wameweza kujiajiri kwani wapo walioanzisha viwanda vidogo vya ufyatuaji matofali,usindikaji wa nafaka,huduma ya chakula na wengine wanafanya ufugaji wa kuku ambao wanafikia takribani mia tano ambapo wamebadilika kiuchumi na baadhi yao wameanza kujenga.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti