• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Waandishi wa Habari wapata mafunzo ya usalama mahala pa kazi

Posted on: September 19th, 2018

Waandishi wa Habari kutoka mikoa saba ya Kanda ya Ziwa, wamepatiwa mafunzo ya namna wanavyoweza kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha usalama wao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Akitoa taarifa  wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa  (UNESCO) Tanzania Dr. Moshi Kimizi alisema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari husasani wa vijijini kuhusu njia bora za kufanya kazi zao kwa ufanisi,  usalama na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini .


"Katika nchi mbalimbali duniani waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi,  takwimu zinaonyesha kwamba, duniani mwandishi mmoja anauwawa kila baada ya siku tano katika harakati za kutekeleza majukumu yake ya kiuandishi ambapo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waandishi 73 walipoteza maisha kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita,"alisema Kimizi.


Aliongeza kuwa, katika baadhi ya nchi duniani, mamia ya waandishi wa habari wanauawa, wanatekwa, wanatishwa, wananyamazishwa, wanadhalilishwa na kuwekwa chini ya ulinzi bila kufuata sheria kwa sababu ya kusema ukweli kwa kueleza maovu mbalimbali yanayoidhuru jamii husika, ndiyo chachu iliyowafanya  UNESCO kuandaa mafunzo hayo.

"Mtajifunza na kujadili mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha uandishi wenu katika mtazamo wa usalama ambapo, baadhi ya mada nyeti zikiwa ni kujifunza sheria za uandishi wa habari, maadili ya uandishi wa habari, sheria za habari za kimataifa ambazo Tanzania inazitambua, sera za vyombo vya habari, bima kwa waandishi wa habari na namna nyingine za kuhakikisha usalama wao pamoja na mikataba ya ajira, hivyo baada ya mafunzo hayo kila mmoja  atayatafasiri kwa vitendo ili kuepukana na habari zinazoweza kuwaletea madhara," aliongeza.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Warioba Sanya ambaye alizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella alisema, suala la usalama na ulinzi kwa waandishi ni lenye umuhimu  hasa ukizingatia majukumu mahasusi waliyonayo ya kuahabarisha ,kuuelimisha na kuushawishi umma  kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii.

Alisema, pamoja na umuhimu huo wa waandishi, takwimu na taarifa za mashirika mbalimbali husasani UNESCO zinaonyesha kuwa takriban waandishi 820 wanauawa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita wakati wakitimiza majukumu yao ,ili kufahamu njia bora zinazopatikana kwa urahisi Serikali kwa kushirikiana na tume hiyo imechukua uamuzi  mahsusi wa kufanya uwezeshaji na  kuendesha mafunzo hayo.

" Nimetaarifiwa mafunzo hayo yatafanyika hapa Mwanza na huko Dodoma yakishirikisha waandishi kutoka takriban mikoa yote ya Tanzania ambapo kwa hapa wametoka Mwanza, Shinyanga, Tabora, Geita, Mara, kagera na Simiyu hivyo matumaini yangu kwa kupitia  mafunzo haya tunaweza kuona mabadiliko makubwa katika sekta ya uandishi wa habari husasani usalama na ulinzi wakiwa kazini," alisema Sanya.

Kwa upande wake mmoja wa wakufumzi wa mafunzo hayo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kupitia shule kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC)  Dotto Kuhenga alisema, mara nyingi waandishi wa habari wanasahau ulinzi na usalama wao wakati wa majukumu yao hivyo ni wakati kutambua na kuzielewa njia za kujilinda dhidi ya hatari yoyote inapojitokeza ili kupunguza ongezeko la waandishi kupoteza maisha.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti