• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

TEHAMA kutatua changamoto Mkoa wa Mwanza

Posted on: January 23rd, 2018


Wabunifu wa TEHAMA kutatua changamoto mbalimbali Mkoa wa Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amefungua kikao cha wabunifu wa Tehama katika kutatua baadhi ya  changamoto zinazoukabili Mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika Ukumbi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiwa ni juhudi zake za kukuza ubunifu na kukabiliana na changamoto mbalimbali nchini, ambapo kikao hicho kimefadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi(COSTECH) kwa kushirikiana na (Atamizi) DTBi, ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa kuibua vipaji vya ubunifu katika Tehama kwa kutumia vijana wabunifu kutoka Mkoa wa  Mwanza.

Kikao hicho kimewapa fursa vijana waliochaguliwa kutatua changamoto mbalimbali za Mkoa wa Mwanza, kuwasilisha mada zao ambazo zina lengo la kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali kwa kutumia matumizi ya Tehama, ambapo kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma, sekta binfsi ( wavuzi, wakulima, wafanyabiashara) CTI, TCCIA, vyombo vya ulinzi na usalama, wataalamu kutotka ngazi ya Mkoa na Halmashauri za Ilemela na Nyamagama.

Suala la usalama ziwani lilichangiwa na wadau wengi kwani asilimia kubwa ya aeneo yanayozunguka ziwa Victoria ni wavuvi hivyo basi, mada iliwasilishwa kwa wadau na kugundua kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili wavuvi na tatizo kubwa ni uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria unahatarisha mazalia ya samaki, pia uhalifu huu huandamana na suala la usalama wa vyombo vya usafiri ndani ya ziwa kwani mara kwa mara wavuvi wamekuwa wanaibiwa injini za vyombo vyao na kunyang’anywa samaki.

 Baada ya kubaini changamoto hizo wataalamu wamekuja na mfumo ambao ni suluhisho la changamoto hizo kwa wavuvi na kwa sasa uko katika hatua za majiribio mara tu utakapokamilika utatumika kutatua shida za wavuvi za kiusalama na hivyo kupunguza na kudhibiti uvuvi haramu na uharamia ziwani.

Mfumo wa kukabiriana na changamoto za foleni za magari barabarani umeshatengenezwa, uko katika hatua za awali za majaribio, inatarajiwa kuwa jeshi la pilisi litatumia mfumo huu utakaobaini magari yasiyofuata sheria barabarani, kubaini ajari barabarani,kwa kuwa kutokana ka kukua kwa Jiji la Mwanza,msongamano wa watu na magari umeongezeka hivyo mfumo huu utatatua tatizo hilo, kwani  watumiaji wataweza kupata taarifa ya barabara zenye msongamono mkubwa na hivyo kutafuta njia mbadala, hii itapatikana kwa kutumia simu za mikononi kwa wale watakaokuwa wamejisajiri kwa mfumo huu.

 Mkoa wa  Mwanza ni miongoni mwa mikoa yenye fursa nyingi katika maeneo ya ufugaji samaki, kuku na kilimo cha mboga mboga na matunda, ubora wa mazao kwa wazalishaji bado uko chini jambo linalowafanya wazalishaji kutokupata masoko ya uhakika yanayowawezesha kukuza kipato chao, hivyo mfumo umeundwa utakaobaini changamto zilizopo katika jiji la Mwanza, na  utasaidia wajasiriamali katika maeneo mbali mbali kupata elimu na majibu ya changamoto zinawakabili hasa katika ufugaji wa samaki, kilimo cha mboga mboga, matunda na ufugaji wa kuku wa kisasa na kienyenyeji.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti