• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wadau wa kilimo,Mifugo,Uvuvi wakutana kutatua changamoto, kuangalia fursa

Posted on: September 19th, 2019


Wadau hao wamekutana leo katika kikao kilichofanyika jijini Mwanza na kuhudhuriwa na taasisi za kifedha, taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya serikali, Makampuni ya huduma za pembejeo na zana za kilimo pamoja na Makampuni ya usindikaji, na kuongozwa na mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John V. K Mongella huku dhumuni likiwa ni kuwakutanisha wadau hao ili kuweza kubadilishana ujuzi wa kazi wanazozifanya.

 Akizungumza katika kikao hicho Mhe.  Mongella amewaeleza wadau hao  kujikita katika kilimo cha mazao ikiwemo kilimo cha alizeti,  pamoja na kilimo cha pamba na kujiuliza  swali, nimefanya nini katika kukuza sekta za kilimo, uvuvi na mifugo.

" Nipende kuwashauri wadau kujikita hasa katika kilimo cha mazao, ikiwemo kilimo cha alizeti mamoja na kilimo cha pamba".

Aidha Mhe.  Mongella amebainisha kuwa sekta ya kilimo imekuwa na mipango ya kuondoa umaskini, kuongeza usalama wa chakula na kuongeza pato.

"Sekta ya kilimo ina mpango wa kuondoa umasikini, kuongeza usalama wa chakula,  ubora wa lishe na kuongeza pato kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, kwenye kaya, jamii mpaka taifa,"alisema Mongella.

 Naye Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio amebainisha kuwa kikao hicho kitatoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa ya kufahamu changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo katika mkoa wa Mwanza.

"Wadau mbalimbali  watapata fursa ya kufahamu changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi katika mkoa wetu wa Mwanza,"alisema Kadio.

Aidha Meneja wa Benki ya NMB tawi la Pamba Road, Dotto Alex Makota, ameeleza kuwa wanashiriki kikamilifu katika huduma za kifedha kwenye kilimo kwa kutoa mkopo wa pesa katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha wakulima wananufaika.

"Sisi kama NMB tunashiriki kikamilifu katika huduma za kifedha kwenye kilimo, na asilimia 35 ya pesa ya NMB inakwenda katika kilimo kwa kutoa mikopo kwa  wakulima," alisema  Makota.

Aidha Mwenyekiti wa wafugaji Wilaya ya Sengerema  Clement Mathayo amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo ikiwemo kukosekana kwa maeneo ya kutosha kwa ajili ya malisho,  maji na  kukosekana kwa soko la uhakika.

"Wadau wa ufugaji tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa soko la uhakika,  maeneo kwa ajili ya malisho na maji, tunaomba Serikali itutazame kwa upana,"lisema Mathayo.

Pamoja na hayo Mhe. Mongella amewashauri viongozi kuweza kutoa nafasi kwa wananchi wao ili kuweza  kuzungumza na kueleza changamoto zinazowakabili katika sekta mbali mbali wakati wa vikao vyao na wananchi, pia amewataka wadau  kuwa mfano kwa kuweza kutekeleza majukumu yao kwa vitendo.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti