• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wafanyabiashara wadogo walalamikia kupanda kwa bei ya sabuni za maji za kunawia mikono

Posted on: March 24th, 2020

Kitendo cha wafanyabiashara kupandisha bei vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na kirusi aina ya Corona ( COVID-19) kimewahathili baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza na kuachana na hali ya kujikinga kwa vifaa .


Hayo yalibainishwa na Nacy Kimaro mkazi wa Mbatini alipokuwa akizungumza na Gazeti hili  alisema kitendo hicho kinachofanywa na wafanyabiashara ni kukomoana kwa sababu wanajua hali ya mtanzania ni duni hivyo walipaswa kuwa wazalendo baada ya kusikia ugonjwa umefika nchini wangeuza kwa bei nafuu kuliko ya awali.


Pia aliiomba serikali kuwapatia vifaa hivyo bure ambapo mtu akiitaji anaenda vituo vya afya na kupatiwa ili mwananchi ambao hawana uwezo wa kununua waweze kuvipata pia mbali na kuvipata elimu itolewa kila mara hasa maeneo ya sokoni ,stend , bar, ili kuwajengea uelewa na kuacha tabia ya kuupuza ugonjwa huu na kuuchukulia ni ugonjwa hatari na utaoweza kuleta maafa .


"Mbona Condom zinagawiwa bure na ukienda  hospitali unazikuta zipo nje unaambiwa uchukue na wakati mwingine daktari anakupatia kabisa kwa nini hivi visipewe bure tena ukizingatia ugonjwa huu ni hatari kuliko magonjwa yote yaliyowahi kutokea na kuuwa watu wengi kwa wakati mmoja" alisema Kimaro.


Naye Kassim Omary mkazi wa Kangae mecco akizungumzia adha hiyo alisema kuingia kwa ugonjwa huo Tanzania imani na uhuru wa kutembea sehemu mbalimbali imepotea hivyo wamejawa na hofu pia kupanda kwa vifaa hivyo imegeuka kuwa changamoto.


Pia alisema,elimu itolewe juu ya matumizi sahihi ya vifaa hivyo na vinapaswa kuvaliwa kwa muda na wakati gani,maana imekua kila mtu anavaa tu kwa utaratibu wake.


" Sisi tunatembea bila kinga yoyote kwanza ukiangalia mimi nina familia ya watu 8 sasa maski moja ni 3000 ambapo kwa siku nitumie labda 28000 kipato changu ni elfu 2000 kwa siku hapo sitoweza bora selikali iingilie kati Rais kazuia mambo mengi yasifanyike kwa ajili ya ugonjwa huu sasa kwa nini hela hiyo isiingie kwenye kununua vifaa vya kujikinga na vigawiwe bure kwa wananchi " alisema Omary.


Naye Bahati Kazimili ni mumiliki na muuzaji   wa duka la madawa Mecco alisema siyo kwamba wanapandisha bei kwa kupenda hiyo inatokana na sehemu wanapochukulia kwa bei ya jumla  kupandisha bei  hivyo kila mtu anaangalia kujiongea kipato .


" Siyo kwamba sisi atuguswi na hili janga lakini mazingira yanatufanya tuuze kwa bei hiyo mfano mwanzo tulikuwa tunatunua boksi moja la maski zikiwa 50 ndani  kwa shilingi 15000 tulikuwa tunaziuza 1500 ambapo kwa sasa tunanunua boksi kwa elfu 80 hivyo inatulazimu kuziuza elfu 3000 kwa kila kimoja "alisema Kazimili.


Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. Thomas Rutachunzibwa alisema wamepokea taarifa ya watu kupandisha bei baadhi ya vifaa hasa wafanyabiashara wa vifaa vya tiba hivyo wamekuwa wakipita na kuwapa elimu ya kutokulichukilia suala hili kama fursa ya kupandisha vitu baadhi wameongea nao na wamewasikiliza.


Aliongeza kuwa kuna wafanyabiashara wengine wanatembeza vitakasa mikono (Hand Sanitizers) mitaani hivyo wamezikamata baadhi na kuzizuia zisitumike.


“Tuhimize wananchi kwamba hii ni vita lakini tunapokuwa tunatumia silaha lazima tuitumie kwa matumizi sahihi na siyo kuichukulia hii kama fursa na kuwaumiza wananchi hasa wale wanaohitaji kununua vifaa kwa bei nzuri lakini wanashindwa kutokana na bei kuwa juu “alisema  Rutachunzibwa.



Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti