• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wakazi 395 wa Mwanza waishio kwenye miinuko kunufaika na mifumo rahisi ya Maji Taka

Posted on: June 7th, 2022


Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya wanatekeleza Ujenzi wa Mfumo rahisi wa Maji taka kwenye makazi ya miinuko unaotekelezwa Tshs Bilioni 3.8 unaosaidia kuhifadhi maji taka kwenye matanki maalum na kuyatibu badala ya kumwaga kwenye ziwa Victoria kama ilivyokua awali.


Hayo yamebainika leo Juni 07, 2022 mtaa wa Igogo -Sahara wakati wa ziara ya Mhe Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiambatana na Kamati ya Ulinzi na  Usalama ya Mkoa alipokua akikagua Miradi ya Maendeleo wilayani Nyamaga pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.


Vilevile, kupitia mradi huo kaya 122 zimeundiwa mfumo wa maji safi na umewezesha ujenzi wa njia maalum za kupanda na kushuka kwenye mitaa hiyo ambapo baada ya ukaguzi wake Mhe Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na mradi huo na amewapongeza watekelezaji wa mradi huo wa kisasa wenye ubunifu.


Vilevile, Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoa elimu ya biashara  kwenye vikundi vyote wanavyowakopesha fedha kutoka makundi ya Wanawake, Vijana na wenye ulemavu kwenye Halmashauri hiyo ili kuweka uhai wa vikundi wanavyokopeshwa.


Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo kwenye Mradi wa kikundi cha Vijana watano cha Yuoth Box Media kilichokopeshwa Tshs Milioni 49 mwaka 2021 ambacho kwa sasa kimekuza mtaji hadi kufikia thamani ya Tshs. Milioni 81 huku kikimiliki bidhaa za Habari kupitia Chaneli za mtandaoni za  Yu box Tv na Yu box Studio.


"Hawa wanafanya vizuri ila mimi nimekuja kuona kama kikundi kina afya, je wana taarifa  za mapato na matumizi ya kikundi, wana vitabu vya fedha na wana utaratibu wa kupima maendeleo ya kikundi chao, hapo lazima tujiulize na Maafisa Maendeleo hiyo ndio kazi yetu kuwajengea uwezo", amesema.


Aidha, Mhe. Mkuu wa Mkoa amekagua Ujenzi wa Barabara ya Hesawa-Yatch Makaburini, Tilapia -Vickfish yenye urefu wa Mita 650 liyotekelezwa kwa zidi ya Tshs. Milioni 348 na ameagiza kurekebisha dosari ndogo kwenye  kingo za barabara hizo na kusafisha mazingira.


Akiendelea na ziara yake Mhe Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi kwa ujenzi wa Mradi wa vyumba 06 vya madarasa kwa mfumo wa ghorofa katika shule ya Sekondari Mkuyuni unaotekelezwa kwa Tshs. Milioni  310 utakaosaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kutoka 85 hadi 52 kwa darasa kwani madarasa hayo yatachukua wanafunzi 900.


Baada ya kukagua uhai wa Vilabu vya kupambana na rushwa na dawa ya kulevya katika shule ya msingi Nyegezi msafara wa Mhe Mkuu wa Mkoa ulifika kwenye Mradi wa Anuani za Makazi katika Mtaa wa Kisese kata ya Mkolani.


Kabla ya kukagua ujenzi wa jengo la Benki ya CRDB tawi la Buhongwa wenye thamani ya Tshs. Milioni 500, Ujenzi wa Kituo cha Afya Bulale kata ya Buhongwa wenye thamani ya Tshs Milioni 500 umehitimisha ukaguzi wa miradi wilayani Nyamagana ambapo Mhe. Mkuu wa Mkoa amesisitiza ukamilishaji wa mradi huo kwa wakati ili uanze kuwahudumia zaidi ya wananchi elfu 5 wanaokusudiwa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti