• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

WAKUU WA WILAYA TATU ZA MKOA WA MWANZA WAKABIDHIWA MAGARI MAPYA

Posted on: July 8th, 2024

WAKUU WA WILAYA TATU ZA MKOA WA MWANZA WAKABIDHIWA MAGARI MAPYA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda amekabidhi magari matatu mapya kwa ajili ya Wakuu wa Wilaya za Ilemela, Misungwi na Sengerema, yenye thamani ya Tsh. milioni 684 ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo.

Akiongea leo katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mtanda amesema anamshukuru Mhe.  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuruhusu na kuidhinisha fedha kwa ajili ya kuwapatia Wakuu wa Wilaya vitendea kazi.

"Sisi Wakuu wa Mikoa nguvu yetu kubwa ni Wakuu wa Wilaya na wao wana maeneo yao ya usimamizi, hivyo ukiwa na viongozi hao hodari na wazuri basi kazi yangu pia itakua nyepesi, hivyo ninawapongeza  wote kwa uchapaji kazi licha ya kutokuwa na vitendea kazi". Mkuu wa Mkoa.

Aidha Mtanda ametoa wito kwa madereva wa magari hayo kuhakikisha wanayafanyia ukaguzi  kila mara baada ya kutembea kilomita elfu 50 na wawapatie taarifa viongozi wao mara baada kufikisha kilometa hizo ili wawaruhusu wakafanye ukaguzi wa magari (Service) hali ambayo itapelekea kuviimarisha vyombo hivyo.

"Na nyie madereva hata kama Mkuu  wako wa kazi atasema tusafiri tu mwambie hapana tufanye service ya gari kwanza , na nyie viongozi wasikilizieni madereva wenu, wakiwaambia gari haiwezi kusafiri msiwalazimishe maana hao ndio wataalamu wa vyombo hivyo". Amesisitiza Mtanda wakati wa makabidhiano hayo

"Msipofanya hivyo mtaisababishia hasara Serikali kwani imetumia na kuwekeza fedha nyingi katika kuwaleteeni ninyi vitendea kazi hivi na nchi hii ina wakuu wa Wilaya wengi ambao bado wana uhitaji wa magari". Mhe.Mtanda

Kadhalika Mkuu huyo wa Mkoa amesema ikiwa tunaelekea katika harakati za uchaguzi, shughuli zitakua ni nyingi kwa Wakuu wa Wilaya zikiwemo za ufuatiliaji, usimamizi, na ukaguzi hivyo amesema atajielekeza pia katika kuhakikiaha Wakuu wa Wilaya za Magu na Ukerewe na wao wanapatiwa vitendea kazi ili kurahisisha utimizaji wa majukumu yao.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya waliokabidhiwa vitendea kazi hivyo, Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Misungwi amesema kwa takribani miaka 3 amekua akitumia gari tofauti  za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi hivyo kupokea gari hiyo mpya itapelekea sasa gari zile alizokua akitumia zikatumike katika shughuli nyingine.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti