• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wamiliki wa Biashara za Vileo watakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Uendeshaji Biashara

Posted on: May 22nd, 2023

*Wamiliki wa Biashara za Vileo watakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Uendeshaji Biashara**


Katika kuhakikisha kwamba biashara za Vileo zinafanyika kwa amani na utulivu, Wamiliki wa Biashara hizo wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za uendeshaji wa biashara hizo kwani kwa kukiuka kufanya hivyo na kuzalisha  kelele sumbufu, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za Baraza  la Taifa la Usimamizi wa Mazingira NEMC.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya llemela Mhe.Hassan Masalla, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo Mai 22, 2023  katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, alipokutana na Vyombo vya Habari.

 Mhe.Hassan Masalla amebainisha kuwa Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na NEMC Mei 5, 2023 walifanya zoezi maalum la kaguzi 50 za wafanyabishara za Vileo na kubaini maeneo 31 ya biashara za vileo  kwenda kinyume na Sheria na kuchukuliwa hatua na kupewa maelekezo namna ya kudhibiti kelele hizo sumbufu.

"Ndugu zangu waandishi nawaomba muwaelimishe vyema wananchi kuhusiana na Sheria na Kanuni za kudhibiti kelele sumbufu, baadhi yetu tumekuwa siyo rafiki na hali hii kutokana na sababu mbalimbali, Serikali inaheshimu taratibu zote zilizowekwa, Biashara hizi zilizobainika kukiuka Sheria zimepigwa faini kati ya Milioni 2 hadi 5 huku zikiendelea kutoa huduma nyingine kama kawaida," amefafanua Mhe.Masalla.

Aidha, amebainisha kuwa maeneo ya biashara za vileo zilizotozwa faini ya Shilingi Milioni 5 ni zile zilizobainika kuwa sugu kwa kuzalisha kelele sumbufu licha ya kuonywa mara kadhaa,na sasa zimetakiwa kuweka vifaa maalum vya kudhibiti kelele hizo.

"Tumejitahidi kuwapa ellimu ya kutosha licha ya kuwapa adhabu kwa mujibu wa kanuni zetu,tunashukuru sasa wamepata uelewa mzuri ili mwisho wa siku kusiwepo na kero kati ya anaye starehe na aliyepo nje na eneo la starehe,"Jerome Kayombo,Meneja Mkoa NEMC.

Aidha Mhe.Masalla amesema zoezi la ukaguzi wa nyumba za ibada litafuata baada ya kukamilika taratibu maalum kwani siyo rahisi kufanya kwa pamoja kaguzi za sehemu za vileo na nyumba za ibada.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti