• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Wananchi Wilayani Magu wahimizwa kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi

Posted on: July 14th, 2022


Viongozi wa Wilaya ya Magu wametakiwa  kuhakikisha kuwa wananchi wanajiandaa vema katika zoezi la sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23 2022, huku Elimu kuhusu Sensa imetakiwa kuendelea kutolewa maeneo mbalimbali ili ifikapo mwezi Agosti wananchi wote wawe wamepata taarifa.

Hayo  yamebainishwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Stergomena Tax wakati akitoa salamu za mwenge wa Uhuru katika viwanja vya Kisasa mapema hii leo.

"Taarifa zote zitakazokusanywa wakati wa Sensa zitakuwa ni kwa malengo ya maendeleo ya Nchi na si vinginevyo niwaombe elimu iendelee kutolewa ili ifikapo Agosti 23 elimu iwe imefika hadi maeneo ya vijijini,"amesema Mhe. Tax.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe.Salum Kalli awali akiwasilisha salamu za Wilaya ya Magu kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Ndugu  Sahili Nyanzabara  Geraruma   amemtaka Kiongozi huyo kumfikishia Salamu za Shukurani Mhe.Rais kwa kuendelea kutuletea fedha za miradi mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya,Maji na Miundombinu ya barabara.

Mhe.Kalli ameahidi usimamizi mzuri wa miradi yote na kusisitiza kuwa Mhe.Rais ana imani kubwa na viongozi aliowapa dhamana hivyo wasimuangushe.


"Ndugu Geraruma tupelekee salaam za Shukurani za wana Magu kwa Mhe.Rais kwamba sisi wana Magu tunashukuru sana kwa kuendelea kutuletea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya yetu, tunaahidi kuendelea kusimamia vema miradi tunayopewa," amesema Mhe.Kalli.

Naye  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Marry Masanja amesema hatawavumilia watendaji kazi wasioendana na kasi ya Mhe.Rais. kwa kuwa Mhe. Rais analeta fedha nyingi sana kwa ajili ya maendeleo hivyo hatuna budi kusimamia kikamilifu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe. Destery Kiswaga amewahimiza wananchi wote wa magu kushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ili kuiwezesha Serikali kupanga maendeleo kwa kwa kuzingatia idadi ya watu.

Hata hivyo, Ziara ya Mwenge wa Uhuru imeingia katika siku ya tatu mkoani Mwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu ambapo Mwenge wa Uhuru

umezindua miradi 3,kukagua miradi 2 na kuweka jiwe la msingi mradi 1 yote ikiwa na thamani ya shilingi bilioni 1.02 ambapo kesho, Julai 15 itakabidhiwa Wilaya ya Ilemela na utakuwa umekamilisha kilomita 120 tokea ukimbizwe Wilaya ya Magu.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti