• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Watumishi watakiwa kuzingatia sheria wakati wa maninuzi

Posted on: May 5th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, amewataka watumishi wa Umma mkoani humo kuzingatia misingi ya uadilifu na uzalendo wakati wanaopojishughulisha kwenye michakato ya ununuzi kwenye taasisi zao ili kuwezesha kupatikana kwa thamani ya fedha kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya Sheria, Kanuni, Miongozo na Mifumo ya Ununuzi wa Umma kwa watendaji na watumishi wa umma kutoka taasisi zilizopo mkoani humo. Mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao katika kutekeleza majukumu yao ya Ununuzi kwenye taasisi zao kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma.

Mhe. Mongella amesema maendeleo ya Halmashauri za mkoa huo yanategemea sana ufanisi wa watumishi hao katika kutekeleza shughuli za Ununuzi  kwa kufuata Sheria na Kanuni za Ununuzi wa Umma ambazo, pamoja na mambo mengine, zinataka wadau wote wanaohusika kwenye michakato ya ununuzi kuzingatia misingi ya uadilifu na uzalendo.

Lazima tuzingatie misingi ya uadilifu na uzalendo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na kuunga mkono azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Niseme tu kwamba hata kwenye Mkoa wa Mwanza, ikithibitika ukosefu wa uadilifu na uzembe wa wazi kabisa kwa watumishi wetu lazima hatua kali zichukuliwe dhidi yao, alisema Mhe. Mongella.

Aidha, Mhe. Mongella alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma zilizomo mkoani humo zinafanya ununuzi wote kwa kuzingatia na kutumia Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya kielektoniki (TANePS) ili kutekeleza matakwa ya Sheria pamoja na maagizo ya Serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri wa PPRA, Mhandisi Mary Swai, alisema kupitia mafunzo hayo washiriki watafundishwa kuhusu matumizi sahihi ya utaratibu wa force account ambao taasisi nyingi za umma huutumia sana wakati huu.

Tunafahamu kwamba utaratibu wa Force Account umekuwa na changamoto kadhaa katika utekelezaji wake, ingawa njia hii ilianza kutumika kwa lengo zuri la kupunguza gharama. Baadhi ya changamoto ni usimamizi hafifu wa miradi unaotokana na wasimamizi kukosa ujuzi wa masuala ya ujenzi. Pia, kutowezeshwa gharama za usimamizi pamoja na kukosa uadilifu kwa baadhi ya wasimamizi, alisema Mhandisi Swai.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamehudhuriwa na takribani washiriki 100 wakiwemo Wajumbe wa Bodi za Zabuni, Wakuu wa Idara Tumizi (user departments, watumishi kutoka vitengo vya Usimamizi wa ununuzi, Wanasheria, na Wakaguzi wa Ndani kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza na taasisi mbalimbali za mkoa huo.  

PPRA imeshaendesha mafunzo kama haya kwenye mikoa 15 nchini, Ruvuma, Njombe, Iringa, Kagera, Shinyanga, Kigoma, Geita, Rukwa, Katavi, Tabora, Mbeya, Dodoma, Songwe, Mara na Simiyu, ambapo huu wa Mwanza ni wa 16.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti