• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa azitaka Halmashauri zote nchini kutunga Sheria rafiki kwa Wachimbaji wadogo wa Madini

Posted on: May 9th, 2023

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb)  amezitaka Halmashauri  zote kutunga sheria ambazo zitakua ni rafiki kwa wachimbaji  wadogo wa madini kwa kuhakikisha wanashirikiana  na wadau katika mapendekezo ya utungaji wa sheria ndogo ndogo.

Mhe. Majiliwa ameyasema hayo leo Mei 9, 2023   alipowasili Jijini Mwanza kwa ajili ya ufunguzi wa  Kongamano la Wachimbaji Wadogo wa Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa Madini (FEMATA)  ambalo limefanyika  katika ukumbi wa Rock City Mall.

" Nawaelekeza Mameya wa Halmashauri nyie ndio mnaotunga sheria ndogo muwe mnahakikisha mnawashirikisha  wadau katika mapendekezo ya utungaji wa sheria ndogo ili msiwe mnatunga sheria ambazo zitakuwa zinawaumiza watumiaji wa sheria hizo," Amesema Mhe. Majaliwa

" Sekta ya madini imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kongamano hili lina fursa kubwa kwetu katika kuzitoa changamoto zetu ili kuongeza tija katika kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta ya madini," Ameongeza Mtendaji Mkuu huyo wa Serikali.

Aidha Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa akizungumza kwa niaba ya  Waziri wa Madini  Mhe. Dkt Dotto Biteko  amemuahidi Mhe. Majaliwa kuwa   Wizara yake  itaendelea kupokea  na kusimamia mikakati inayotolewa na serikali.

" Mhe. Waziri Mkuu nakuahidi kuwa Wizara itaendelea kupokea na kusimamia  mikakati  inayotolewa na serikali ili kuhakikisha inaongeza kasi katika kuchangia maendeleo nchini," Amesema Mhe. Dkt. Kiruswa

Pia  Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mwaza ameiomba Wizara ya Madini na Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa Madini (FEMATA) kuja kufanya kongamano lijalo la Mwaka 2024 mkoani humo

" Mhe. Mgeni rasmi kama kauli mbiu yetu inavyosema kwamba amani iliyopo  Tanzania itumike kuwa fursa ya kiuchumi na Tanzania kwa kitovu cha biashara ya madini Afrika tunaiomba serikali iunde chombo maalum ambacho kitashughulika na suala la amani ili kukuza uchumi," Amesema  Ndg. John Binna,Rais wa FEMATA

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa  amefungua kongamano hilo la  Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa Madini (FEMATA) ikiwa ni maagizo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti