• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Waziri Silaa ampongeza RC Makalla kwa kusimamia na kutatua migogoro ya ardhi Mwanza

Posted on: December 5th, 2023

Waziri Silaa ampongeza RC Makalla kwa kusimamia na kutatua migogoro ya ardhi Mwanza


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa yupo kwenye ziara fupi Mkoani Mwanza na kumpongeza Mkuu wa Mkoa huo Mhe.CPA.Amos Makalla kwa kusimamia na kutatua vyema migogoro ya ardhi ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Akizungumza leo kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi kutoka sekta ya ardhi, Mhe Silaa ameweka bayana kuwa huo ni mfano wa kuigwa kwa watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia eneo hilo kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi  na kuzingatia sheria za ardhi.

"Migogoro mingi inaonesha dhahiri chanzo ni sisi baadhi yetu tunaopindisha taratibu zilizopo kwa tamaa binafsi na kuwaacha wananchi wakitaabika na kudhulumika, hilo kama Waziri mwenye dhamana sitalifumbia macho,"amesisitiza Waziri Silaa wakati akizungumza na watumishi kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara yake na wengine kutoka Halmashauri.

Amesema Mhe.Makalla amelazimika kutoka ofisini na kwenda kujionea kero zinazowarudisha nyuma kimaendeleo wananchi wake na kuzitolea maamuzi, nyingi zikiwa ni migogoro ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya watumishi waliokosa nidhamu ya kazi na badala yake kukimbilia kujinufaisha

"Haiwezekani sheria ziwekwe halafu wengine wanazitii na baadhi kuzipuuzia tena kwa kukusudia huo siyo utaratibu unaokubalika na nitahakikisha uzingatiaji wa sheria za nchi unaheshimika,"Silaa

Waziri Silaa ametoa maagizo kwa kamishna msaidizi wa ardhi Mkoa wa Mwanza Bi.Happines Mtutwa kuhakikisha mkazo wa elimu,ufuatiliaji,na utatuzi wa kero kwa wananchi unafanyika mara kwa mara

Awali kabla ya kikao hicho Waziri Silaa alipata wasaa wa kupata taarifa fupi za mkoa wa Mwanza hasa masuala ya ardhi kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi anaye kaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti