• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 23 WA KATA YA KAGUNGULI UKEREWE WAPATA MAJI SAFI

Posted on: October 8th, 2024

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 23 WA KATA YA KAGUNGULI UKEREWE WAPATA MAJI SAFI


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Godfrey Eliakim Mnzava amezindua mradi wa maji Bukindo- Kagunguli (Tanki la Maji Kagunguli) wenye  thamani ya Tshs. Bilioni 2.3 chini ya usimamizi wa wakala wa maji na usafi wa mazingira mjini na vijini (RUWASA).

Akizungumza na wananchi baada ya uzinduzi wa mradi huo leo Oktoba 8, 2024 uliojengwa na mkandarasi Otonde construction co ltd. Ndugu Mnzava amewataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwasaidia kwa muda mrefu.

Aidha, kiongozi huyo ameiagiza jumuiya ya watumia maji kuhudumia wananchi kwa haki na usawa kwa kuzingatia bei ya maji inayoweza kuhimilika na mwananchi mwenye kila hali ya uchumi ili malengo ya kuipatia jamii maji safi na salama yatimie kwa wote.

"Naomba tuutunze mradi wetu na miundombinu yake ili iweze kutuhudumia kwa muda mrefu na tusimvumilie mtu atakayetaka kuhujumu lakini pia jumuia ya watumia maji siku zote tuhudumie jamii kwa usawa na haki kwenye bei kwa kuhakikisha inakua rafiki kwa wote."

Awali, Kaimu Meneja wa RUWASA wilaya ya Ukerewe Mhandisi Flowin Mkechi amesema mradi huo unahusisha matenki mawili ya maji yenye ujazo wa lita 150,000 na kwamba wananchi elfu 23.2 kutoka kwenye vijiji vya Buzegwe, Nampise, Muhande na Buguza katika kata  ya Kagunguli vimefikiwa na mradi huo.

Halikadhalika, kiongozi huyo wa mbio za mwenge mwaka huu amemkabidhi Bi. Khadija Nyankubi nyumba ya kisasa aliyojengewa na wadau kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa huo la kumpatia zawadi bibi huyo mzalendo aliyetoa eneo la ujenzi wa mradi huo bila kudai fidia.

Katika wakati mwingine, Mwenge wa Uhuru wilayani Ukerewe umezindua mabweni 3 ya kidato cha V na VI, madarasa 8 na matundu 33 ya vyoo vyenye thamani ya tshs. Milioni 694.2 katika shule ya sekondari Bukondo ambapo Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Emanuel Bomba ameishukuru Serikali kwa miundombinu hiyo.


Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti