• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Balozi India avutiwa fursa za Tanzania

Posted on: September 23rd, 2019


Balozi  wa India nchini, Mhe. Sanjiv Kohli amesema  taifa lao linafurahishwana  namna Tanzania inavyotoa fursa  na kuwalinda wawekezajinchini kitendo ambacho kimeendelea kuwa kivutio kwao.

Kauli hiyo ameitoajana mkoani Mwanza katika mkutano wa pamoja kati ya  wafanyabiashara  waIndia waishio Tanzania na wanachama wa  Chemba yaWafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoa wa Mwanza.

Kohli alisema tangumwaka 1990 hadi 2018, India imeweza kuwekeza miradi mbalimbali Tanzania ambayoinafikia Dola za Marekani bilioni 2.21 sawa na Sh trilioni 5.5 zaTanzania  na kutoa ajira  zipatazo 55,000 katika miradi   424.

“India ni ya taifala  tano katika uwekezaji wa miradi hapa Tanzania ikitanguliwa naChina, Uingereza, Marekani na  Mauritius,  ukiwa India ukiulizamfanyabiashara yeyote anataka kuwekeza wapi, ataanza kuitaja Tanzania, hii niishara kwamba ni kivutio.

“Binafsinathibitisha wazi India na Tanzania tumekuwa katika ushirikiano tangu mwaka1972 ambapo hadi kufikia 2018, jumla ya wanafunzi 500 wamesomea na kupatamafunzo mbalimbali, hata katika mkutano huu wapo waliosemea kule na kuja kuwaviongozi.

“Hapa Tanzania ipobaadhi ya miradi ambayo tumeitekeleza  na hata kutoa misaada katikaChuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vikiwamo DIT sambamba na  hospitaliya Bugando, vile vile ipo miradi ya maji kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze,mradi wa maji wa vijiji 89 vya mkoa wa  Tabora katika wilayaza  Nzega na Igunga,”alisema  

Balozi Kohlialisema baada ya kuteuliwa kuja Tanzania amefurahi kuona wafanyabiashara waIndia wakiendelea na shughuli zao  nchini bila kuwa na kikwazochochote ambapo aliahidi kuhamasisha matajiri wa taifa lao kuja kuwekeza zaidi.

Alisema baadhi yamiradi waliyowekeza nchini hawajawahi kupata hasara jambo ambalo linathihirishaushirikiano uliodumu tangu mwaka 1972, hivyo aliwahakikishia masoko kwa baadhiya bidhaa ambazo Tanzania imekuwa ikitegemea soko India.

Naye Katibu Tawalawa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo,John Mongella alimuomba  na kumhakikishia balozi huyo kwamba Tanzaniainawakaribisha wawekezaji na kuwalinda kwa namna yoyote  ili kilaupande uweze kunufaika ambapo alianisha uwekezaji unaohitahitajika kwa sasa nisekta ya kilimo na  viwanda  vya kuzalisha bidhaambalimbali.

Kadioalisema  moja ya mikoa yenye fursa  katika uwekezaji niMwanza ambayo ni kitovu cha nchi za Afrika Mashariki  kutokana nauwezo wa ardhi ya kutosha, ziwa viktoria, madini, hifadhi za taifa za wanyamana mzunguko  mkubwa wa fedha.

“Mwanza tunaendeleakutekeleza sera ya Tanzania ya uwekezaji ndio maana tunawakaribisha wawekezajikwa kuwa  ardhi tunayo tena ya kutosha ikizingatiwa mkoa wetu ndiokitovu cha nchi za Afrika Mashariki, kupitia uwepo wa balozi wa India hapa,tunamuomba awaweleze watu wake wawekeze hasa katika viwanda, kampuni zauhandisi, hoteli na sekta ya kilimo nayo inahitaji uwekezaji.

“Ukiwekeza Mwanzaunakuwa umejiweka katikati ya soko la nchi za Afrika Mashariki, uhakika upo wakile unachokizalisha kununuliwa ukizingatia Serikali ipo kwenye utekelezaji wakuboresha miundombinu ya majini na nchi kavu  sambamba na vyombo vyausafiri ikiwa lengo ni kuondoa changamoto ya mawasiliano yaliyokuwapoawali,”alisema.

Kwa  upandewa Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA), Mkoa wa Mwanza, Dk. Elibariki Mmari alisema lengo la kukutanishwawafanyabiashara wa India na Tanzania ni  kujifunza na kupata uzoefuwa kujenga miradi mikubwa.

Dk. Mmarialisema  raia wa India wamepiga hatua katika   masualaya teknolojia  hasa upande wa uhandisi hivyo ni matarajio kwawatanzania kutumia fursa ya kushirikiana na kupata uzoefu wa ujenzi wa madarajamakubwa nchi kavu na majini, majengo marefu aina ya maghorofa.

“India na Tanzaniazimekuwa katika mahusiano ya miaka mingi hakujawahi kutokea hali ya kuteterekauhusiano wa  kidiplomasia ndio maana unaona wafanyabiashara wan chihizo mbili wamekuwa na ushirikiano sana katika shughuli zao.

“Indiaimekuwa  ni moja ya taifa ambalo linanunua  kwa wingibidhaa kutoka Tanzania ambazo ni pamba, korosho, dengu, madini aina ya dhahabuna almasi, hivyo hivyo na sisi watanzania tumekuwa tunaagiza vitu kutoka Indiaambavyo  ni  nguo, dawa, gari na huduma zakibenki,”alisema.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti