Ndugu Msomaji karibu katika Tovuti rasmi ya Mkoa wa Mwanza. Historia ya mkoa wa Mwanza ilianza wakati ukiwa chini ya tawala za kitemi za wasukuma, wazinza, walongo, wakara na wakerewe kabla ya ukoloni. Wajerumani walipotawala Tanganyika eneo la Mwanza likawa mojawapo ya wilaya katika himaya ya utawala wa Kijerumani.
Utawala wa kikoloni wa Mwingereza ulipokabidhiwa uangalizi wa Koloni la Afrika Mashariki baada ya vita kuu ya Dunia, ulianzisha utawala wa majimbo yaani Provinces. Tanganyika ilikuwa na majimbo ya kiutawala manane (8) na mojawapo likiwa ni Lake Province.
Lake Province liliundwa kwa kujumuisha maeneo ya wilaya za Mwanza, Biharamulo, Bukoba, Maswa, shinyanga, Musoma na Kwimba. Baadaye Lake Province liligawanywa na kuunda majimbo mawili la Lake Province (Sukuma Land) na Western Province). Utawala wa Mwingereza ulimalizika na Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.
Baada ya uhuru Mwanza iliendelea kuwa sehemu ya Jimbo la Lake Province chini ya mtawala wake kwanza wa jimbo (Provincial Commissioner) aliyeitwa Provincial Commissioner Bw. Walden, ambaye alikabidhi madaraka kwa Richard Wambura.
Mkoa wa Mwanza ulianzishwa rasmi mwaka 1963 ukiwa na wilaya nne za Ukerewe, Geita, Mwanza na Kwimba. Mwaka 1972 baada ya sera ya madaraka mikoani wilaya zaidi zilianzishwa kwa kuanza na Magu mwaka 1974. Wilaya ya Sengerema ilianzishwa mwaka 1975 ambapo awali ilikuwa ni tarafa mojawapo ya wilaya ya Geita.
Misungwi ilianzishwa mwaka 1995 ambapo awali ilikuwa ni eneo la tarafa za wilaya ya Kwimba, Ilemela na Nyamagana zilianzishwa mwaka 2002 ambazo zilikuwa zinaunda wilaya ya Mwanza. Mwaka 2010 mikoa mipya ya Geita na Simiyu ilitangazwa kuanzishwa. Wilaya mpya pia za Busega na Nyanghwale nazo zilitangazwa kuanzishwa 2010 na utekelezaji wake utaanza rasmi wakati wowote katika mwaka wa fedha 2011/12.
Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania.Mipaka ya Mkoa, Mkoa wa Mwanza unapakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.
Idadi ya watu, kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2. Wilaya ndizo Ukerewe,Magu, Sengerema,Geita,Misungwi,Kwimba,Nyamagana na Ilemela. Jiji la Mwanza ndani yake lina wilaya za Nyamagana na Ilemela.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
Buchosa : mbunge ni Dk. Charles Tizeba (CCM)
Ilemela : mbunge ni Angelina Mabula (CCM)
Kwimba : mbunge ni Mansoor Hirani (CCM)
Magu : mbunge ni Kiswaga Boniventura (CCM)
Misungwi : mbunge ni Charles Kitwanga (CCM)
Nyamagana : mbunge ni Stanslaus Mabula (CCM)
Sengerema : mbunge ni William Ngeleja (CCM)
Sumve : mbunge ni Richard Mganga Ndassa (CCM)
Ukerewe : mbunge ni Joseph Mkundi (Chadema)
Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.
Makabila ya Mkoa wa Mwanza
Makabila makubwa katika Mwanza ni Wasukuma kwa wilya za Sengerema, Magu, Kwimba, Misungwi na Ilemela ili hali Wilaya ya Nyamagana wanaishi makabila tofauti tofauti na wilya ya Ukerewe hupatikana Wakerewe na na Wakara.
Historia ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala walio wahi kuongoza Mkoa wa Mwanza
Wakuu wa Mikoa walioongoza Mkoa wa Mwanza toka 1961 hadi sasa.
NA
|
Jina Kamili
|
Mwaka alionza
|
Mwaka alioondoka |
1.
|
Mhe. Richard Wambura
|
1961
|
1963
|
2.
|
Mhe. J Samwel Malecela
|
1963
|
1965 |
3.
|
Mhe.Joseph Nyerere
|
1965
|
1967 |
4.
|
Mhe.Joseph Namata
|
1967
|
1969 |
5.
|
Mhe.Omary Muhaji
|
1969
|
1972 |
6.
|
Mhe.Lawi Sijona
|
1972
|
1975 |
7.
|
Mhe.Peter Kisumo
|
1975
|
1977 |
8.
|
Mhe.Muhidin Kimario
|
1977
|
1979 |
9.
|
Mhe.Abdulnuru Suleiman
|
1979
|
1981 |
10.
|
Mhe.Daniel Machemba
|
1981
|
1987 |
11.
|
Mhe.Timoth Shindika
|
1987
|
1992 |
12.
|
Mhe.Philip Mangula
|
1992
|
1993 |
13.
|
Mhe.Ernest Nyanda
|
1993
|
1994 |
14.
|
Mhe.Dkt.William Shija
|
1994
|
1995 |
15.
|
Mhe.Mj. Gen.James Luhanga
|
1996
|
1999 |
16.
|
Mhe.Stephen Mashishanga
|
1999
|
2003 |
17.
|
Mhe.Daniel Ole Njolai
|
2003
|
2006 |
18.
|
Mhe.Dkt Eng.James Allex Msekela
|
2006
|
2009 |
19.
|
Mhe. Abbas H. Kandoro
|
2009
|
2011 |
20.
|
Mhe.Eng.Evarist W. Ndikilo
|
2011
|
2014 |
21.
|
Mhe.Magessa S. Mulongo
|
2014
|
2016 |
22.
|
Mhe.John V.K Mongella
|
2016
|
2021
|
23.
|
Mhe. Albert Chalamila
|
2021
|
2021
|
24.
|
Mhe. Eng. Robert Gabriel
|
2021
|
2022 |
25. | Adam K. Malima | 2022 | 2023 |
26. | CPA. Amosi Makalla | 2023 | Mpaka sasa |
Makatibu Tawala Walioongoza Mkoa wa Mwanza toka 1972 hadi sasa
NA. |
Jina Kamili |
Mwaka alioanza |
Mwaka alioondoka |
1. |
C. Y. Mpuya |
1972 |
1975 |
2. |
R. Ringo |
1975 |
1977 |
3. |
W. K. Kasera |
1977 |
1981 |
4. |
W. H. Shelukindo |
1981 |
1983 |
5. |
J. R. Kyambwa |
1983 |
1984 |
6. |
E. O. Oluoch |
1984 |
1987 |
7. |
M. D. Mapunda |
1987 |
1990 |
8. |
J. K. Kyambwa |
1990 |
1995 |
9. |
R. R. Kiravu |
1995 |
1997 |
10. |
C. M. Rutaihwa |
1997 |
2006 |
11. |
Alh. Y. Mbila |
2006 |
2009 |
12. |
Doroth S. Mwanyika |
2009 |
2013 |
13. |
D. Faisal H. H. Issa |
2014 |
2016 |
14. |
C.P.Clodwig M. Mtweve |
2016 |
2018 |
15. | Christopher Derek Kadio
|
2018 | 2020
|
16.
|
Emmanuel M. Tutuba
|
2020
|
2021
|
17. | Ngusa D. Samike | 2021 | 2022 |
18.
|
Balandya M. Elikana | 2022
|
Mpaka sasa |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.