• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi Yahamasishwa Mwanza

Posted on: May 6th, 2019

Jumla ya wanawake 50,000 hapa nchini kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hupata maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi na hivyo kusababisha asilimia 37 ya wanawake wanaogundulika na ugonjwa kufariki kila mwaka.


Hayo yamesemwa  jijini hapa na Afisa Mpango  wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na watoto  Pricella Kinyunyi alipokuwa akieleza lengo mahususi la serikali kuanzisha chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri kuanzia miaka 9- 14 kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya afya kutoka wilaya zote za mkoa wa Mwanza.


Alisema wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi hawapati mapema huduma za ugunduzi na matibabu sahihi kwa wakati hali inayosababisha vifo.


“Takwimu kutoka hosipitali ya ocean Road inaonyesha  kwamba, saratani ya mlango wa Kizazi inachangia kwa asimilia 36 ya saratani zote na asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi wanajitokeza katika hatua ambayo tayari saratani imesha sambaa maeneo mengine mwilini,” alisema.  


Aliongeza kuwa chanjo hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani na kwamba majaribio ya matumizi ya chanzo kwa mara ya kwanza yalianzia mkoani Kilimanjaro mwaka 2014 na haikuwa na madhara ya kiafya.


“Matokeo ya chanjo hiyo yalikuwa ni mazuri mkoa ulifikia asilimia 90 ya uchanjaji, lengo hasa lilikuwa ni kupata uzoefu wa kujifunza kwa vitendo kabla ya kwenda nchi nzima,” aliongeza.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela katika kuhakikisha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi unatokomezwa, amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji na wenyeviti wa halmashauri kuhakikisha wanahamasisha vijana wengi kwenye maeneo yao ili waweze kupata chanjo hiyo.


“ Hatuwezi tu kuruhusu watu kupata huduma za tiba peke yake, lazima tuhakikishe program za chanjo katika mkoa wetu zinaimarishwa,” alisema.


Kwa mujibu wa taarifa za serikali, mkoa wa Mwanza umetekeleza zoezi la chanjo ya kuzuia  saratani ya mlango wa kizazi ambayo ilizinduliwa rasmi April 23 mwaka jana, na kuandikisha jumla ya mabinti 31,291 wenye umri chini ya miaka 14, ambapo uliweza kuchanja jumla ya mabinti 24,628 ikiwa ni sawa na asilimia 79 ya ufanisi.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti