• barua pepe
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Wasiliana Nasi
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government
Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Mwelekeo
    • Historia ya Mkoa
    • Muundo
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Idara
    • Utawala na Rasilimali Watu
    • Planning and Management
    • Fedha na Uhasibu
    • Ukaguzi wa Ndani
    • ununuzi na Ugavi
    • Uchumi na Uzalishaji
    • Miundombinu
    • Serikali za Mitaa
    • Social Welfare
    • Tehama
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
  • Investments
    • Investment One
    • Investment Two
    • Investment Three
    • Investment Four
    • Investment Five
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya Picha
    • Sports and Games
    • Hotuba
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Maktaba ya Video

CHF iliyoboreshwa itolewe elimu - RC Mongella

Posted on: October 16th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa kutembelea Halmashauri zote za Mkoa ili kutoa elimu kwenye mabaraza ya madiwani juu ya faida na gharama za bima ya afya ya jamii ya CHF.

Mhe.Mongella alitoa agizo hilo kwenye kikao cha ushauri cha Mkoa (RCC)kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo na kujumuisha wajumbe mbalimbali, na kuongeza kuwa  kutohamasisha wananchi kujiunga na mifuko ya bima za afya ni dhambi.

"Chukua timu yako nenda kwenye Halmashauri zetu zote kaa na CMT wala hatapoteza kitu chochote kwenda kutoa mafunzo kwenye mabaraza ya madiwani,mkatoe uelewa wa suala hili," alisema Mhe. Mongella.

Aliongeza kuwa  Ofisi za ma-DMO watoe  elimu ili kuwapa wananchi faida za bima ya afya ikiwemo unafuu wa gharama za afya kwani  bima ya afya ni mkombozi kwa wananchi.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa alisema wapo  kwenye mchakato wa CHF mpya na kumba  hawajasitisha CHF ya zamani ikiwemo bei ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambayo ni sh.10,000.

"Kama kuna aliyesitisha ni makosa, CHF ya zamani inaendelea mpaka hapo tutakapokamilisha maandalizi ya CHF iliyoboreshwa, hakuna barua iliyotoka kwa Katibu Tawala Mkoa  ikisimamisha, bado tunaendelea na utaratibu wa zamani "alisema Dkt. Rutachunzibwa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe.  Sharif Mansoor alisema alitaka kukata bima za wananchi zaidi ya 3000 lakini juhudi zake zikashindikana kwa kuwa na mkanganyiko wa gharama kwani awali ilikuwa sh.10,000 ila akaambiwa sh.30,000.

Hata hivyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhe. Renatus Mulunga alisema wameishaanza kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida za bima ya afya.

"Kwa Manispaa ya  Ilemela tumeisha elimisha wananchi juu ya CHF iliyoboreshwa kwa utaratibu ni watu sita wa familia moja watalipia sh.elfu 30,000," alisema Mhe. Mulunga.

Latest Announcements

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali.

    soma zaidi
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025

    soma zaidi
  • View More

Habari Mpya

  • SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA: UKEREWE YAPATA AJIRA 127
  • RC MTANDA AWASILI WILAYANI UKEREWE KWA ZIARA YA KIKAZI
  • MWANZA YAIMARISHA UTETEZI WA WATU WENYE ULEMAVU
  • SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU WA SEKTA YA BIASHARA
  • CHOROKO KWENYE RAMANI YA UCHUMI WA TAIFA
  • soma zaidi

Wasiliana Nasi

Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Balewa/Machemba Road Street
S.L.P: S.L.P 1333, Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Simu ya Mkononi: 0768520195
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
S.L.P: S.L.P 735, Mwanza
Simu: + 255 736 200910
Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz
Simu ya Mkononi:
Halmashauri ya Wilaya ya Magu
S.L.P: S.L.P 200, Magu
Simu: 028-2530035/2530003
Barua Pepe: ded@magudc.go.tz
Simu ya Mkononi:

Viunganishi vya Haraka

  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Fomu ya Ugonjwa
  • Opras fomu
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • FFARS User Guidelines
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Salary Slips Portal
  • Tovuti ya Sekreatarieti ya Ajira Tanzania
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Rasmi ya Wananchi
  • Tovuti Kuu ya Takwimu Huria

Social Media

  • Like us on Facebook
  • Follow us on Twitter
  • Find us on Youtube
  • Follow us on Instagram

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.

  • Kanusho
  • Sera ya faragha
  • Maswali ya Mara kwa Mara
  • Ramani ya Tovuti